SERIKALI YAAHIDI KUTATUA KERO ZA WAUGUZI NA WAKUNGA NCHINI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, March 20, 2024

SERIKALI YAAHIDI KUTATUA KERO ZA WAUGUZI NA WAKUNGA NCHINI


Na Hamida Ramadhan , Dodoma


SERIKALI imekiri kuwa inatambua mchango mkubwa wa watumishi kutokana sekta ya afya hasa wakunga na wauguzi kwa juhudi kubwa wanayofanya licha ya changamoto zilizopo katika Kada hiyo.

Naibu Waziri wa Afya Dkt,Godwin Mollel
wakati wa kikao kazi cha kufanya tathimini ya utekelezaji wa utendaji kazi wa utoaji wa huduma za uuguzi na Ukunga zoezi lililoenda sambamba na uzinduzi wa jarida la idara ya Uuguzi na Ukunga jijini Dodoma.


Amesema licha ya changamoto za kimiugozo ,kifedha na kimiundo wanazokumbana nazo wauguzi na wakunga lakini bado wamekuwa wakifanya kazi zao kwa umakini na weledi

"Ni ukweli usiopingika asilimia 60 ya watumishi katika sekta ya afya nchini wanatoka kada za uuguzi na ukunga na wamekuwa wakichangia ubora wa huduma katika Hospitali na Vituo vya kutolea huduma za afya licha ya kuwepo kwa changamoto ya kimiundo kimiundo na haha kifedha ," Amesema Waziri Dkt. Mollel

Dkt. Mollel amesema kada ya Uuguzi imekuwa muhimu katika kutoa huduma bora kwa sababu asilimia 80 ya kazi za afya zinatekelezwa na kada hiyo na kutoa rai kada hiyo kujumuishwa kwenye mfumo wa utoaji wa maamuzi.

Vile vile amemshukuru Rais kwa kutoa fedha ambazo zimepelekea watumishi kufundishwa na kuongeza u juzi , vifaatiba kuongezeka katika hospital na vituo vya afya bila kusahau fedha hizo kukarabati miundombinu.

"Uwekezaji huu wa fedha kutoka wa Rais Dkt, Samia Suluhu Hassan vituo vimejengwa, watumishi wamejengewa uwezo vifa tiba vimeongezeka na miundombinu kuboreshwa, " Amesema Dkt Mollel

Kwa upande wake Mkurugenzi wa idara ya Huduma za Uuguzi na Ukunga Ziada Sella ameishukuru Serikali kupitia Wizara ya Afya kwa kuajiri Wauguzi na Wakunga zaidi ya 40,000 kwa kipindi cha mwaka 2022/2023 na kuongeza kuwa kada hiyo ina dhamana kubwa katika utoaji wa huduma hivyo wazingatie miongozo, kanuni na sheria zilizowekwa kwa maslahi ya taifa.

“Tunamshukuru Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa kibali cha kuajiri wauguzi na wakunga zaidi ya elfu arobaini hii inaonyesha umuhimu na dhamana ya kada hii kwa sababu hawa ndio hutumia muda mwingi kukaa na wagonjwa.

Kikao hicho kilichowakutanisha Viongozi wauguzi na Ukunga kote nchini kimebeba kauli Mbiu isemayo “Huduma Staha na Mawasiliano ni Wajibu wa Kila Mtoa Huduma za Afya”.

Naye Rais wa Chama cha wauguzi na Manesi Alexander Bulanya amesema Wakunga na wauguzi ndio uti wa mgongo wa utoaji wa huduma ya afya nchini na hiyo wathaminiwe na kuangaliwa kwa jicho la pekee.

Amesema serikali imekuwa ikitoa ufadhili wa kimasomo ya kibobezi nje ya nchi lakini changamoto wanayokutananayo baada ya kumaliza masomo hayo muudo kutowatambua

" Tunaomba serikali ilione hili hasa mwaka fedha katika kupitisha bajeti na hili lipendekezwe kwani ni changamoto ya muda mrefu sasa, " Amesema Bulanya


No comments:

Post a Comment