TANROADS WAENDELEA NA KAZI KUREJESHA MAWASILIANO YA BARABARA SOMANGA - MTAMA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, March 25, 2024

TANROADS WAENDELEA NA KAZI KUREJESHA MAWASILIANO YA BARABARA SOMANGA - MTAMA


Timu ya wataalamu kutoka Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) wanaendelelea na kazi ya kurejesha mawasiliano ya barabara katika eneo la Somanga - Mtama kilometa 220 kutoka Mkoani Lindi kutokana na daraja linalounganisha barabara kuu ya kutoka Dar es Salaam na Mikoa ya Pwani, Lindi na Mtwara kukatika na kusababisha barabara hiyo kufungwa.

Akitoa taarifa leo tarehe 25 Machi 2024 Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa ameeleza kuwa jitihada kubwa zinaendelea za kurudisha mawasiliano ya barabara katika eneo hilo.

“Timu za TANROADS kutoka Mikoa ya Lindi na Pwani zimeungana kuongeza nguvu ili kabla ya mchana safari ziweze kuendelea. Tunawapa pole wasafiri wote kwa changamoto iliyojitokeza”, ameeleza Waziri Bashungwa.



Kwa upande wao Meneja wa TANROADS wa Mikoa ya Lindi na Pwani Mha. Emil Zengo na Mha. Baraka J. Mwambage wamesema wanafanya kila jitihada kurejesha mawasiliano ya barabara hiyo haraka ili ili Wananchi waweze kuendelea na shughuli zao za uzalishaji.

No comments:

Post a Comment