Na Mwajuma Mlewa ,OKULY BLOG,Dodoma
Ameyasema hayo katika hafla fupi ya kukabidhi magari na pikipiki kwa wizara na taasisi zinazotekeleza program ya kuendeleza kilimo na uvivu (AFDP) iliyofanyika katika mji wa serikali mtumba Jijini Dodoma yenye lengo la kusaidia ukuzaji wa viumbe maji na kuleta tija kwa wakulima.
Aidha ameeleza kuwa program hiyo imeanza utekelezaji wake katika kusaidia kuleta mabadiliko kwenye kuzalishaji na uendelezaji wa biashara kwa kuzingatia mazingira halisi ya kilimo cha kisasa na wafanya biashara wadogo wadogo kwenye sekta ya uvuvi.
"Tukio hili la leo ni moja ya hatua muhimu sana katika utekelezaji wa program ya (AFDP) na mafanikio makubwa tunayo yataraji katika program hii,na sisi tunaamini kama kila mmoja wetu ambae yupo hapa atasimamia vizuri program hii na kufanya ufatiliaji wa karibu bila shaka manufaa makubwa ya kimaendeleo yataifanya nchi yetu iweze kupiga hatua Kubwa,
Na kuongeza kuwa "Kwa kazi nzuri hii iliyofanywa na viongozi wetu wakuu wa nchi na sisi hatuta lala usiku na mchana kuhakikisha matunda yanayo tarajiwa kupatikana kwenye program hii yanapatikana kwa haraka sana na yana wanufaisha wananchi wote wa Tanzania na hasa wanawake na vijana katika kutibu tatizo la Ajira nchini,"
Hata hivyo amebainisha kuwa watendaji wakuu wa wizara na taasisi husika wanatakiwa kuwa na usimamizi mzuri wa matumizi ya vifaa vya moto kwa kufanya ufuatiliaji wa mara kwa mara katika utekelezaji wa miradi mbalimbali.
"Mara nyingi tumeshuhudia magari ya taasisi mbalimbali yameachwa yakiharibika bila kufanyiwa ukarabati na Mradi huu utakwenda takribani miaka sita na tunaamini magari haya niya kudumu,magari tunayoyatoa leo na yatakayo endelea kutolewa yanaendelea kufanya kazi ndani ya serikali na kuleta tija katika serikali yetu,"
Sambamba na hayo jumla ya pikipiki 23 (tatu zikiwa ni za miguu mitatu),na magari 11 yenye thamani ya zaidi ya billion 2 yamekabidhiwa kwa taasisi na wizara zinazotekeleza program hii,ambapo Ofisi ya waziri mkuu gari 1,Wizara ya kilimo (gari moja),Wizara ya mifugo na uvuvi (magari manne na pikipiki 16-tatu zikiwa za miguu mitatu),Taasisi ya utafiti wa kilimo-TARI (magari mawili na pikipiki 4), na wakala wa mbegu za kilimo-ASA (magari matatu na pikipiki 3).
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. David Silinde alisema vifaa hivyo vitaenda kuchochea kasi ya utekelezaji katika sekta ya kilimo hasa katika shughuli mbalimbali zilizopangwa katika utekelejazi wa program hiyo na kutoa rai kwa taasisi zote zilizo chini ya Wizara hiyo zinahakikisha vifaa hivyo vinatumika kwa malengo yaliyokusudiwa ili kuweza kufikia malengo ya Programu.
No comments:
Post a Comment