"FORCE ACCOUNT HAINA SHIDA,TATIZO NI WASIMAMIZI KUKOSA UMAKINI " DKT. NCHEMBA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Tuesday, March 12, 2024

"FORCE ACCOUNT HAINA SHIDA,TATIZO NI WASIMAMIZI KUKOSA UMAKINI " DKT. NCHEMBA

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), akizungumza wakati wa hafla ya Uwekaji Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Jengo la Taaluma la Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) Kampasi ya Dodoma, katika eneo la Njedengwa, jijini Dodoma. Jengo hilo la ghorofa Sita lenye ukubwa wa takribani Sqm 6600, litakuwa na uwezo wa kuhudumia wanafunzi ya 4,500 kwa wakati mmoja.
Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA), Dkt. Mwamini Tulli, akizungumza wakati akimkaribisha Mgeni rasmi Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb) kutoa hotuba yake, wakati wa hafla ya Uwekaji Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Jengo la Taaluma la Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) Kampasi ya Dodoma, katika eneo la Njedengwa, jijini Dodoma, ambapo Mwenyekiti huyo ameishukuru Wizara ya Fedha kwa kuwapa ushirikiano katika utekelezaji wa majukumu ya msingi ya Chuo ya kutoa mafunzo, kufanya tafiti na kutoa ushauri wa kitaalam.
Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA), Prof. Eliamani Sedoyeka, akizungumza wakati wa hafla ya Uwekaji Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Jengo la Taaluma la Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) Kampasi ya Dodoma, katika eneo la Njedengwa, jijini Dodoma, ambapo amesema kuwa Ujenzi huo unaoendelea unafanywa kwa kutumia mapato yake ya ndani kupitia wataalam wa ndani yaani ‘Force Account’.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb) (kushoto), akikata utepe katika hafla ya Uwekaji wa Jiwe la Msingi la Jengo la Taaluma la Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) Kampasi ya Dodoma, katika eneo la Njedengwa, jijini Dodoma. Jengo hilo la ghorofa Sita lenye ukubwa wa takribani Sqm 6600, litakuwa na uwezo wa kukalisha wanafunzi 4,500 kwa wakati mmoja. Wengine katika picha ni Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo hicho, Dkt. Mwamini Tulli, Mkuu wa Chuo hicho, Prof. Eliamani Sedoyeka na Mbunge wa Arusha Mjini, Mhe. Mrisho Gambo.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), akikagua ujenzi unaoendelea wa Jengo la Taaluma la Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) Kampasi ya Dodoma, baada ya kuweka Jiwe la Msingi, katika eneo la Njedengwa, jijini Dodoma. Jengo hilo la ghorofa Sita lenye ukubwa wa takribani Sqm 6600, litakuwa na uwezo wa kuhudumia wanafunzi ya 4,500 kwa wakati mmoja.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb) (wa pili kushoto), akizungumza na Mbunge wa Arusha Mjini, Mhe. Mrisho Gambo (katikati) wakati akikagua ujenzi unaoendelea wa Jengo la Taaluma la Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) Kampasi ya Dodoma, baada ya kuweka Jiwe la Msingi, katika eneo la Njedengwa, jijini Dodoma. Jengo hilo la ghorofa Sita lenye ukubwa wa takribani Sqm 6600, litakuwa na uwezo wa kukalisha wanafunzi ya 4500 kwa wakati mmoja. Wengine katika picha ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary Senyamule (kushoto) na Mkuu wa Chuo hicho, Prof. Eliamani Sedoyeka.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb) (Katikati walioketi), Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary Senyamule (watatu kulia walioketi), Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo hicho, Dkt. Mwamini Tulli (watatu kushoto walioketi), Mbunge wa Arusha Mjini, Mhe. Mrisho Gambo (wa kwanza kushoto walioketi), Kamishna wa Idara ya Sera za Ununuzi wa Umma kutoka Wizara ya Fedha anayemwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Fredrick Mwakibinga (wapili kulia walioketi) na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Dodoma, Bi. Sakina Mbughi (wa kwanza kulia walioketi), na Mkuu wa Chuo hicho, Prof. Eliamani Sedoyeka, wakiwa katika picha ya pamoja na Menejimenti ya Chuo hicho baada ya hafla ya Uwekaji wa Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Jengo la Taaluma la Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) Kampasi ya Dodoma, katika eneo la Njedengwa, jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb) (Katikati walioketi), Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary Senyamule (watatu kulia walioketi), Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo hicho, Dkt. Mwamini Tulli (watatu kushoto walioketi), Mbunge wa Arusha Mjini, Mhe. Mrisho Gambo (wa kwanza kushoto walioketi), Kamishna wa Idara ya Sera za Ununuzi wa Umma kutoka Wizara ya Fedha anayemwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Fredrick Mwakibinga (wapili kulia walioketi) na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Dodoma, Bi. Sakina Mbughi (wa kwanza kulia walioketi), na Mkuu wa Chuo hicho, Prof. Eliamani Sedoyeka, wakiwa katika Picha ya pamoja na Timu ya wataalam wa ujenzi wa jengo hilo baada ya hafla ya Uwekaji wa Jiwe la Msingi la Jengo la Taaluma la Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) Kampasi ya Dodoma, katika eneo la Njedengwa, jijini Dodoma.

Na Okuly Julius-Dodoma

Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Nchemba amesema matumizi ya fedha za mapato ya ndani kupitia wataalamu wa ndani yaani “ Force Acount” katika ujenzi wa miradi mbalimbali hapa nchini sio tatizo ili tatizo ni kukosekana kwa wasimamizi makini wa miradi hiyo.

Amesema dhamira ya Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Awamu ya sita wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni kuona watanzania wanashikilia uchumi wa nchi yao wenyewe kwa kushiriki katika Nyanja zote za maendeleo ikiwemo miradi mikubwa ya ujenzi wa miundombinu na sio kutegemea wataalamu kutoka nje ya nchi na mwisho wao faida yote wanapeleka katika mataifa yao.

Dkt.Nchemba ameyasema hayo leo Machi 12,2024 Jijini Dodoma ,wakati wa hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi jengo la taaluma katika Kampasi ya Dodoma ya Chuo Cha Uhasibu (IAA) inayojengwa na chuo hicho kwa kutumia fedha za mapato yake ya ndani kupitia wataalamu wa ndani yaani “Force Account”

“Tulipoanza kutumia Force Accout watu wakaanza kupiga kelele ila niwaambie ukweli Force Account haina tatizo lolote ila tatizo ni kukosekana kwa wasimamizi makini wenye uzalendo ndio maana miradi ilikuwa inasuasua na mengine wanatekeleza chini ya kiwango ila hapa IAA wanatuonesha jinsi Force Account inavyoweza kutumika na ikaleta matokeo mazuri.

Na kuongeza kuwa “dhamira ya Dkt. Samia ni kuona watanzania wanashikilia uchumi wa nchi yao wenyewe sasa tunapokosa usimamizi mzuri katika miradi yetu na wataalamu wetu kutoshiriki katika miradi mikubwa dhamira hii nzuri ya Rais wetu itakuwa ni bure kwani Watanzania tutaendelea kuwa nyuma na wageni wataendelea kufurahia kuchuma na kupeleka maendeleo katika mataifa yao sisi huku tunabaki kuwa watazamaji wakati serikali imeweka kila aina ya jitihada za kushirikisha watanzania katika ujenzi wa uchumi wa nchi” amesema Dkt. Nchemba

Dkt.Nchemba ameuagiza uongozi wa chuo hicho kukuendelea kusimamia kwa ukaribu ujenzi wa jengo hilo na kuzingatia viwango vya ubora,sheria ,taratibu na miongozo ya matumizi ya fedha za umma na kukamilisha miradi hiyo kwa wakati na kuonesha thamani halisi ya fedha.

Amesema matarajio ya Serikali katika ujenzi wa miundombinu ya elimu kama madarasa ,kumbi za mihadhara ,maktaba maabara za kompyuta unaeendelea katika kampasi zote za Chuo cha Uhasibu (IAA) zitaleta chachu katika kutoa elimu bora kwa wananchi.

“Miundombinu hii itawawezesha kuwaandaa wataalam mahiri kwenye fani za Uhasibu,Benki,Fedha ,uchumi,usimamizi wa rasilimaliwatu,ununuzi na ugavi ,usimamizi wa biashara ,utalii ,masoko na maeneo mengine watakakokidhi mahitaji ya soko la ajira wakiwa na ujuzi na maarifa ya kukabiliana na changamoto za kijamii na kiuchumi,” ameeleza Dkt.Nchemba

Kwa upande wake Mkuu wa Chuo cha Uhasibu (IAA) Prof. Eliamani Sedoyeka amesema jengo hilo lina ghorofa sita na litakuwa na madarasa ,ofisi,maktaba, na maabara ya kompyuta ambapo likikamilika litakuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi 4500 kwa wakati mmoja.

Amesema katika miaka miwili ijayo Chuo hicho kinatarajia kukamilisha Jengo Kuu (Campus Main Building) ambapo litawezesha Kampasi ya Dodoma kudahili wanafunzi 7,806 kwa mwaka.

“Napenda kutoa wito kwa wanafunzi wetu watarajiwa kuchangamkia fursa ya kujiunga na Chuo chetu ili kujenga mustakabali wao kwa kujifunza na kukua kitaalamu , na tutajitahidi kufanya kila linalowezekana kuwawezesha kufikia malengo yao ya elimu na kazi,” amesema Prof. Sedoyeka

Naye Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi la Chuo Cha Uhasibu Arusha (IAA), Dkt. Mwamini Tulli, aliipongeza Serikali kwa kuendelea kuunga mkono Chuo hicho katika ujenzi wa miundombinu ya elimu kwa lengo la kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia ambapo katika kipindi cha miaka miwili shilingi bilioni tatu (03) zilipokelewa kwa ajili ya ujenzi unaoendelea katika Kampasi ya Arusha na Kampasi ya Babati.

Aliahidi kuwa Chuo kitaendelea kusimamia matumizi ya fedha hizo na kuhakikisha kuwa zinafanya kazi iliyokusudiwa pamoja na kuhakikisha kwamba Chuo chao kinatoa wahitimu wenye weledi na ujuzi unaohitajika katika kuleta maendeleo ya taifa.


Chuo cha Uhasibu Arusha kinaendelea na ujenzi wa jengo la Taaluma litakalokuwa na uwezo wa kuhudumia wanafunzi 4,500 kwa wakati mmoja, kwa kutumia mapato yake ya ndani kwa kutumia wataalam wa ndani (Force Account) na linatarajiwa kukamilika mwezi Julai na litaanza kutumika mwezi Oktoba, 2024.

No comments:

Post a Comment