Tanzania na Ujerumani zimesaini Makubaliano ya ahadi (commitment) ya msaada wa kiasi cha euro milioni 70 (sawa na shilingi bilioni 193.71) kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo nchini Tanzania, ikiwemo Sekta za maji, Afya, Maliasili, Utawala Bora na Usimamizi wa Sheria.
Makubaliano hayo yametiwa saini Jijini Dar es Salaam na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bw. Elijah Mwandumbya na Mkuu wa Idara ya Afrika Mashariki, Wizara ya Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo ya Ujerumani, Bw. Marcus Von Essen.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, Bw. Elijah Mwandumbya, amezipongeza timu za wataalam wa nchi hizo mbili kwa kazi ya kuongoza majadiliano yaliyowezesha kukubaliana na kusainiwa kwa Kumbukumbu za Majadiliano hayo, ambazo zinaelezea ushirikiano wa nchi hizo kwa maendeleo ya wananchi wa Tanzania.
Bw. Mwandumbya, ameishukuru Serikali ya Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani kwa ahadi ya msaada huo utakaozinugausha sekta za maendeleo nchini katika eneo la Bioanuwai, ambalo kwa kiasi kikubwa linajumuisha kusaidia Hifadhi za Taifa na Hifadhi za Wanyamapori ili kuhifadhi mazingira yake tajiri ya asili na kuongeza mapato kupitia utalii endelevu, pia katika Sekta ya Afya ambayo inajumuisha maeneo ya Huduma za Dharura za Watoto Wachanga, Afya ya Uzazi na Uzazi wa Mpango kwa vijana, na Bima ya Afya ya Pamoja.
“Kwa niaba ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ninatoa uju shukrani zangu za dhati kwa msaada huu ninawahakikishia kwamba, Serikali ya Tanzania itafuatilia kwa karibu ili kuhakikisha kwamba fedha zinatumika kama ilivyokusudiwa” alisema Bw. Mwandumbya.
Aliongeza kuwa ahadi zilizotajwa zitasaidia miradi maalum ikiwemo wa Kupunguza Migogoro baina ya Binadamu na Wanyama , kiasi cha Euro milioni tisa (9); Mradi wa Maendeleo Endelevu ya Mifumo ya Hifadhi, kiasi cha euro milioni 15, Mradi wa Kuimarisha Afya ya Uzazi na Kuwawezesha Vijana wa kike, kiasi cha euro milioni tisa na Mradi wa Kuimarisha Mfumo wa Bima ya Afya wa kwa Wote nchini Tanzania, kiasi cha euro milioni tatu (3).
Alisisitiza kuwa maeneo mengine ni Mradi wa Kuanzisha Bima ya Afya ya Pamoja, kiasi cha euro milioni 15, Mradi wa Upatikanaji wa Haki kwa Wanawake na Watoto, kiasi cha euro milioni sita (6), Mradi wa Kuzuia unyanyasaji wa Kijinsia, kiasi cha euro milioni 10, Mradi wa Utawala Bora na Usimamizi wa Fedha, kiasi cha euro milioni mbili (2) na Fedha kwa ajili ya maandalizi ya miradi, kiasi cha euro milioni moja (1).
“Ningependa kuthibitisha tena dhamira ya Serikali ya Tanzania chini ya uongozi wa Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya kuendelea kuimarisha ushirikiano wetu muhimu kwa ajili ya maendeleo ya watu wetu,” aliongeza Bw. Mwandumbya.
Kwa Upande wa Mkuu wa Idara ya Afrika Mashariki, Wizara ya Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo ya Ujerumani, Bw. Marcus Von Essen, ameishukuru Tanzania kwa kuendelea kudumisha Ushirikiano wao katika maendeleo ya maeneo muhimu yanayogusa wananchi moja kwa moja.
“Tumekuwa na uaminifu na ushirikiano mzuri sana kati yetu, tumeangalia vipaumbele katika ushirikiano wetu na tumezungumza kuhusu namna ya kuongeza kasi katika majadiliano yetu ili mafanikio ya mazungumzo haya yaonekane kwa haraka” alisema Bw. Essen.
Bw. Essen aliongeza kuwa, Ujerumani itaendelea kufanya kazi na Serikali ya Tanzania kwa ajili ya maendeleo ya watu wa Tanzania.
Kwa upande wake Balozi wa Ujerumani nchini, Mheshimiwa Thomas Terstegen, alizishauri pande zote kuendelea kushirikiana kwa karibu ili kuhakikisha malengo ya maendeleo endelevu yanafikiwa kama ilivyokusudiwa.
Alisema miradi iliyotajwa inatekelezwa chini ya dhamira ya Serikali inayoongozwa na Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, inayolenga kuendelea kuimarisha ushirikiano kwa maendeleo ya wananchi.
Mwisho.
Captions
PIX 1
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, Bw. Elijah Mwandumbya (Kulia) kwa niaba ya Serikali ya Tanzania na Mkuu wa Idara ya Afrika Mashariki, Wizara ya Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo ya Ujerumani, Bw. Marcus Von Essen (katikati) kwa niaba ya Serikali ya Shirikisho la Ujerumani, wakitia saini hati za Makubaliano ya ahadi (commitment) ya msaada wa kiasi cha euro milioni 70 (sawa na shilingi bilioni 193.71) kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo nchini Tanzania, ikiwemo Sekta za maji, Afya, Maliasili, Utawala Bora na Usimamizi wa Sheria, katika hafla iliyofanyika katika Ukumbi wa Hazina Ndogo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Balozi wa Ujerumani nchini, Mhe. Thomas Terstegen.
PIX 2
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, Bw. Elijah Mwandumbya (Kulia) kwa niaba ya Serikali ya Tanzania na Mkuu wa Idara ya Afrika Mashariki, Wizara ya Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo ya Ujerumani, Bw. Marcus Von Essen (katikati) kwa niaba ya Serikali ya Shirikisho la Ujerumani, wakibadilishana Hati za Makubaliano ya ahadi (commitment) ya msaada wa kiasi cha euro milioni 70 (sawa na shilingi bilioni 193.71) kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo nchini Tanzania, ikiwemo Sekta za maji, Afya, Maliasili, Utawala Bora na Usimamizi wa Sheria, katika hafla iliyofanyika Ukumbi wa Hazina Ndogo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Balozi wa Ujerumani nchini, Mhe. Thomas Terstegen.
PIX 3
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, Bw. Elijah Mwandumbya (Kulia) kwa niaba ya Serikali ya Tanzania na Mkuu wa Idara ya Afrika Mashariki, Wizara ya Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo ya Ujerumani, Bw. Marcus Von Essen (katikati) kwa niaba ya Serikali ya Shirikisho la Ujerumani, wakionesha Hati za Makubaliano ya ahadi (commitment) ya msaada wa kiasi cha euro milioni 70 (sawa na shilingi bilioni 193.71) kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo nchini Tanzania, ikiwemo Sekta za maji, Afya, Maliasili, Utawala Bora na Usimamizi wa Sheria, katika hafla iliyofanyika Ukumbi wa Hazina Ndogo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Balozi wa Ujerumani nchini, Mhe. Thomas Terstegen.
PIX 4
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, Bw. Elijah Mwandumbya (Kulia) kwa niaba ya Serikali ya Tanzania, akizungumza baada ya hafla ya utiaji saini Hati za Makubaliano ya ahadi (commitment) ya msaada wa kiasi cha euro milioni 70 (sawa na shilingi bilioni 193.71) kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo nchini Tanzania, ikiwemo Sekta za maji, Afya, Maliasili, Utawala Bora na Usimamizi wa Sheria. Hafla hiyo imefanyika katika Ukumbi wa Hazina Ndogo, jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mkuu wa Idara ya Afrika Mashariki, Wizara ya Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo ya Ujerumani, Bw. Marcus Von Essen.
PIX 5
Mkuu wa Idara ya Afrika Mashariki, Wizara ya Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo ya Ujerumani, Bw. Marcus Von Essen (katikati), akizungumza wakati wa hafla ya utiaji saini hati za Makubaliano ya ahadi (commitment) ya msaada wa kiasi cha euro milioni 70 (sawa na shilingi bilioni 193.71) kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo nchini Tanzania, ikiwemo Sekta za maji, Afya, Maliasili, Utawala Bora na Usimamizi wa Sheria. Hafla hiyo imefanyika katika Ukumbi wa Hazina Ndogo, jijini Dar es Salaam. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, Bw. Elijah Mwandumbya na Kushoto ni Balozi wa Ujerumani nchini, Mhe. Thomas Terstegen.
PIX 6
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, Bw. Elijah Mwandumbya (wa tatu Kushoto), Balozi wa Ujerumani nchini, Mhe. Thomas Terstegen (watatu kulia) na Mkuu wa Idara ya Afrika Mashariki, Wizara ya Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo ya Ujerumani, Bw. Marcus Von Essen ( wa pili kulia), wakiwa katika picha ya pamoja na ujumbe kutoka Serikali ya Tanzania na Ujumbe kutoka Shirikisho la Ujerumani, baada ya hafla ya Utiaji saini wa hati za Makubaliano ya ahadi (commitment) ya msaada wa kiasi cha Euro milioni 70 (sawa na shilingi bilioni 193.71) kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo nchini Tanzania, ikiwemo Sekta ya maji, Afya, Maliasili, Utawala Bora na Usimamizi wa Sheria. Hafla hiyo imefanyika katika Ukumbi wa Hazina Ndogo jijini Dar es Salaam.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Dodoma)
No comments:
Post a Comment