Wanafunzi wa Shule ya Msingi Mwongezeko iliyopo Kata ya Kisangura, Wilaya ya Serengeti mkoani Mara wamepatiwa elimu ya usalama barabarani kwa lengo la kuwajengea uwezo wa kukabiliana na changamoto wanazokutana nazo wanapotumia barabara.
Akitoa elimu hiyo, Mkaguzi wa Polisi wa Kata ya Kisangura, Mkaguzi wa Polisi (INSP) Genuine Kimario, amesema wanafunzi hao wamekuwa wakikumbana na changamoto mbalimbali wanapokatiza au kutumia barabara, hivyo akaona ni muhimu kuwapatia elimu hiyo ili kuwasaidia kujilinda na ajali za barabarani.
Ameeleza kuwa katika elimu hiyo wanafunzi wamefundishwa kuhusu sheria na alama mbalimbali za usalama barabarani zitakazowaongoza wanapotumia barabara.
Aidha, amesisitiza umuhimu wa kutambua alama za vivuko vya watembea kwa miguu, akibainisha kuwa wengi wa wanafunzi hao hawakuwa wanazitambua vizuri alama hizo.
Katika hatua nyingine, amewataka wanafunzi kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi kuhusu vitendo vya ukatili wanavyoweza kufanyiwa na watu wasiotaka maendeleo yao ya kielimu, ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi ya wahusika.

No comments:
Post a Comment