WADAU WATAKA AL HILAL IPEWE NAFASI YA KUGOMBEA UBINGWA NBC PREMIER LEAGUE. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Tuesday, March 19, 2024

WADAU WATAKA AL HILAL IPEWE NAFASI YA KUGOMBEA UBINGWA NBC PREMIER LEAGUE.



Umeshawaza msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania bara kutakuwa na ugeni wa moja ya vilabu vikubwa katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati?


Basi kama haujui, ikufikie taarifa kuwa, miamba ya soka nchini Sudan, Al Hilal, watakuwepo katika ligi yetu msimu ujao wakishiriki mwanzo hadi mwisho wa ligi.


Imekuaje mpaka hili linatokea? Ni kwamba kutokana na ligi nchini mwao kusimama kwa muda usiojulikana kwa sababu ya vita, ongozi wa klabu hiyo uliandika barua kwa Shirikisho la Soka nchini (TFF) kuomba nafasi ya kushiriki katika ligi ya Tanzania ili kulinda viwango vya wachezaji wao na kujiweka sawa kwa mashindano ya kimataifa.


Kufuati ombi hilo, TFF wamekubali lakini ushiriki waohautahusisha moja kwa moja msimamo wa ligi, kwa mana ya kwamba, hawatagawiwa alama katika mechi zao kama ilivyozoeleka bali watakuwa kama washiriki wa ligi kwa mtazamo wa mechi za kirafiki.


Licha ya utaratibu huo, wadau wa soka wameomba wajumuishwe katika kinyang'anyiro cha kugombea ubingwa ili upinzani wongezeke maradufu.


Wazee wa majamvi watakuwa wanaangalia mwenendo wa sakata hili, wakifahamu kuwa endapo hawatajumuishwa katika msimamo, kutazaliwa kwa mechi kubwa nyingine baina ya wababe wa Kariakoo na matajiri wa chamazi, hiyo itakuwa fursa ya kupiga pesa kutokana bora wa miamba hiyo.


Wakijumuishwa, mtifuano wa kugombea ubingwa utakuwa mtamu mno. Al Hilal watakuwa wanatafuta ubingwa wao wa kwanza, Yanga na Simba nao hawatataka kupoteza ufalme wao mbele ya mgeni sambamba na kutaka kuendelea kuchukua taji hilo mara nyingi zaidi. Hapa kutakuwa na fedha nyingi za kushinda kama hilo litafanikiwa.

No comments:

Post a Comment