Mtangazaji wa Televisheni ya Afrika Kusini Shamiso Mosaka. |
Mtangazaji wa Televisheni ya Afrika Kusini Shamiso Mosaka aliondolewa kwenye ndege kutoka Durban hadi Johannesburg kwa nguvu kutokana na tabia yake ya "ukaidi", maafisa wanasema.
Shirika la ndege la CemAir lilisema Jumatatu kwamba safari ya ndege ilicheleweshwa kwa dakika 90 kwa sababu ya kukataa kwa mshawishi huyo kufuata "kanuni za usalama". Iliongeza kuwa rubani alilazimika kusimamisha "injini ambazo tayari zilikuwa zimewashwa".
Bi Mosaka hakujibu ombi la BBC la kutaka maoni yake, lakini alirekodi mgogoro huo kwenye Instagram Live.
Mshawishi huyo ana zaidi ya wafuasi 140,000 kwenye Instagram na ni mtangazaji kwenye chaneli ya muziki ya MTV Base ya Afrika Kusini.
Video hiyo imesambazwa sana kwenye mitandao ya kijamii, huku wengi wakiandamana kumuunga mkono Bi Mosaka.
Katika video hiyo mshawishi anaombwa kuondoka kwenye ndege na maafisa wa polisi, lakini anakataa kufanya hivyo hadi watakapoahidi kumwandikia ndege nyingine.
Wafanyakazi wa shirika la ndege wanakataa ombi hili. Anajaribu kujitetea na kujaribu kutafuta usaidizi kutoka kwa abiria wengine ili kuthibitisha kwamba hakuwa msumbufu.
Kisha Bi Mosaka anasema anahisi kisa hicho kimechochewa na ubaguzi wa rangi kwani anadai wafanyakazi wa baraza hilo wameshindwa kueleza ipasavyo alichokosea.
Afisa Mkuu wa Fedha wa CemAir Laura van der Molen aliambia gazeti la ndani la The Citizen kuwa hakuna "maelezo ya rangi".
Alisema kuwa Bi Mosaka "alikataa kuzingatia kanuni za shirika la ndege na kwa bahati mbaya akalazimika kuondolewa kwa nguvu".
Hali hiyo ilitokea Jumapili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa King Shaka Zulu.
CemAir inasema tukio hilo limewasilishwa kwa polisi wa Afrika Kusini na watashughulikia suala hilo.
No comments:
Post a Comment