WAKILI MPANJU AHIMIZA MAKATIBU TAWALA WA MIKOA KUTOA ELIMU YA MALEZI NA MAKUZI BORA YA MTOTO. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, March 18, 2024

WAKILI MPANJU AHIMIZA MAKATIBU TAWALA WA MIKOA KUTOA ELIMU YA MALEZI NA MAKUZI BORA YA MTOTO.


Na Carlos Claudio, Dodoma


Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Amon Mpanju amesisitiza makatibu tawala wa mikoa, wasaidizi wa makatibu tawala, makatibu ustawi wa jamii pamoja na maafisa lishe na elimu kutoa elimu ya malezi na makuzi bora ya mtoto ili watoto wa kitanzania wakue katika muelekeo wa kufikia utimilifu wao sawa na sayansi ya malezi inavyoelekeza.

 

Akizungumza leo Machi 18, 2024 jijini Dodoma katika ufunguzi wa kikao kazi cha siku moja cha uwasilishaji wa viashiria vya malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto (ECDI) kwa mwaka 2030, wakili Amon Mpanji amesema taifa linaenda kutengeneza rasilimali watu wenye tija kwa taifa ambao watakuwa na uwezo wa kufanya kazi na kuleta maendeleo yao wenyewe, jamii pamoja na taifa kwa ujumla.

 

“Wazazi, walezi, jamii na serikali tuweke mifumo ya kuwafwatilia watoto waweze kulelewa sawasawa na sayansi ya malezi na makuzi pia kuzingatia lishe inayotakiwa katika malezi sahihi yanayo shahuriwa kiustawi, kisaikolojia kiafya, uchangamfu na menigine yote ikiwa kupata tiba zote sahihi kwa wakati,”amesema wakili Mpanju.

 

Amesema Kwa mujibu wa sayansi ya malezi na makuzi inaonesha kuwa asilimia 47 ya watoto wenye miezi 24 hadi 59 ndiyo wanaolelewa katika mwelekeo sahihi wa kukua kufikia utimilifu wake ya asilimia ya watoto walio katika mwelekeo sahihi wa kufikia ukuaji timilifu inapungua kadri umri unavyoongezeka kutoka asilimia 36 kwa watoto wa miezi 24 -35 mpaka asilimia 58  kwa watoto wa umri wa miezi 48 -59.

 

Wakili Mpanju amesema,“Kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi yetu viashiria vya malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto vinaingizwa katika utafiti wa taifa wa demografia ya maswala ya afya huku viashiria vya malaria vya mwaka 2030 ambao utafiti huo sasa ulifanyika mwaka 2021/2022  na sasa hivi malengo pekee ni ECDI ya mwaka 2030 lakini kwa mara ya kwanza tumekuwa tukifwata takwimu kwa miaka mingi toka tupate uhuru hivyo viashiria vya malezi na makuzi na maendeleo ya mtoto havijawahi kuwa sehemu ya utafiti ya nchi hii kwaio kwa utafiti uliofanyika wa mwaka 2022 vimeingizwa.”

 

Pia amesema kutokana na tafiti za kuingizwa kwa viashiria hivyo vimeweza kusaidia katika kupata taarifa kamili kwenye kila mkoa juu ya viashiria vya malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto jinsi inavyoenda.

 

Kwa upande wake Mkurugenzi msaidizi huduma za ustawi wa jamii, ofisi ya Rais TAMISEMI Subisya Kabuje amesema serikali inaendelea kutekeleza programu jumuishi ya Taifa ya malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya Mtoto katika kuhakikisha watoto wote nchini wanafikia ukuaji timilifu.

 

“Progamu hii katika awamu ya kwanza imetekelezwa katika mikoa 10 ambayo ni Arusha, Dar Es Salaam, Dodoma, Kagera, Manyara, Morogoro, Lindi, Mbeya, Rukwa na Tabora na washiriki katika mikoa walipata mafunzo, kuanzia Aprili 2023 programu hii ilipanua wigo kwa kuongeza mikoa 16 iliyokuwa imebaki na kufikia mikoa 26,”amesema Kabuye.

 

Amesema katika utekelezaji wa programu hiyo jumla ya vituo 2341 vya kulele watoto mchana vimesajiliwa nchini vinavyohudumia watoto 17492 sambamba na uanzishwaji wa vituo vya kijamii 65 katika mikoa ya Dar Es Salaam, Dodoma na Tanga.

 

Naye Mwakilishi wa shirika la kuhudumia watoto Duniani (UNICEF) Mlemba Abassy, ambaye ni mtawimu, amesema kutokana na utafiti kuwa mchache wataendelea kushirikina na TAMISEMI, ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) pamoja na wadau wengine ili kupata viashiria vingi kuhusiana na malezi, makuzi a maendeleo ya awali mtoto.

 

Programu hiyo muhimu ilizinduliwa na kuheshimiwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania ambapo Mhe. waziri Dkt. Dorothy Gwajima (Mb) Waziri wa maendeleo ya jamii, jinsia, wanawake na makundi maalum aliiwasilisha rasmi programu hiyo mnamo tarehe 13, Disemba 2021.









No comments:

Post a Comment