WANAKIJIJI WA KATA YA LUPETA WAIOMBA SERIKALI KUWALETEA MAJI. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, March 27, 2024

WANAKIJIJI WA KATA YA LUPETA WAIOMBA SERIKALI KUWALETEA MAJI.



Dodoma, Mpwapwa

Wananchi wa kijiji cha kata Lupeta wilaya ya Mpwapwa jijini Dodoma  waiomba serikali kuwaletea maji kwani Kijiji hicho kina changamoto za maji kiasi  wanakosa kutekeleza majukumu yao ya nyumbani pamoja na kuomba kujengewa zahanati.

Hayo yamebainishwa Machi 26, 2024 wakati wa ziara ya  mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Mpwapwa  Yohana Malogo wakati kukagua uhai wa Jumuiya, kusajiri wanachama wapya, kuhimiza ulipaji wa ada pamoja na kukusanya kero na maoni Ili kufikisha sehemu husika.


"kilio cha maji katika kata yetu imekuwa ni changamoto kiasi cha kwamba tunashidwa kuelewa tatizo hili litaisha lini na serikali inampango gani na wananchi wa kata yetu, kumekuwa na vikao vingi sana wakati inakaribia uchaguzi ila mafanikio baada ya kuchaguliwa ni hafifu," amesema mmoja wa wananchi.


Kwa upande wake fundi mkuu wa maji Geogre Francis Theophil amesema kuwa wapo baadhi ya wananchi wanakata mabomba ya maji usiku bila sababu yoyote kiasi cha kwamba wanakwamisha swala la maji kupatikana katika kijiji hicho.

" Tumekuwa tukipokea changamoto nyingi hasa hii laini ya zamani unakuta mtu ana kukata bomba, cha ajabu zaidi huu mradi mpya bomba ni kubwa ila unakuta mtu analikata bomba kwa lengo anikwamishe ili nisionekane nafanya kazi, tunajitaidi usiku tufungulie maji yajae ila unakuta mtu kakata maji yanaishia chini.

Naye Diwani ya kata ya Lupeta Sospeter Moonho amewahakikishia kuwa mradi wa maji tiririka kufika mwezi wa nne utaenda kuendelea ili kusaidiia kumtua mama ndoo kichwani pamoja na kuwahakikishia wananchi wanaenda kuanza ujenzi wa jengo la zahanati.

"Nimekuja kufanya kazi ndani ya miaka mitano mlionipa nitahakikisha huu ujenzi wa jengo la zahanati umekamilika na kama sijakamilisha nitakapokuja kuomba kura tena mniulize maswali ila Jumatatu naenda kuanza ujenzi" amesema  Moonho.


Kwa upande wake mwenyekiti Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi ( UVCCM) Yohana Malogo amewataka viongozi wa kata hiyo kuhakikisha mifuko ya simenti iliyokopeshwa  irudishwe na ujenzi uanze pia amewasisitiza kuwa kisima kijengwe kwenye kata hiyo.


"Tunaenda kwenye serikali za mitaa tuache hizo dhambi za kuwaumiza wanachama tuhakikishe tunawasaidia wananchi kama wananchi washadhulumiwa sana hata hicho kiasi kilichopo ujenzi uanze aina haja ya kuweka fedha wakati wote huku wananchi hawaoni kinachofanyika," amesema Malogo.


Lengo la ziara hiyo ni kukagua uhai wa jumuiya, kukagua madaftari ya wanachama, kusajiri wanachama wapya, ulipaji wa ada, kuhamasisha kufanyika semina kwa viongozi wa kata, mitaa pamoja na kikao Cha ndani kwa wanachama.




No comments:

Post a Comment