Antony amekashifiwa kwa shangwe yake iliyolenga wachezaji wa Coventry City kufuatia ushindi wa Manchester United kwa mikwaju ya penalti kwenye uwanja wa Wembley.
Mbrazil huyo alionekana akitega masikio na kuwakimbia wachezaji kufuatia mkwaju wa Rasmus Hojlund unaowapeleka fainali ya FA itakayochezwa May 25, 2024 katika dimba la Wemnley dhidi ya mahasimu wao kutoka jiji moja Manchester City.
City wamefanikiwa kutinga fainali kwa mchezo mgumu ikimchapa Chelsea kwa goli 1-0, goli lililopachikwa na kiungo Benardo Silva mnamo dakika za 84.
Manchester United wakiwa wanaharakisha ujio wa skauti mkuu Sam Williams huku mipango yao ikiwa inaimarika, Manchester City na Chelsea ni miongoni mwa timu zinazoongoza katika Ligi Kuu ya Uingereza kuhitaki huduma ya kinda wa St Mirren Ethan Sutherland.
No comments:
Post a Comment