Na Carlos Claudio, Dodoma.
Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari imefanikiwa kutambua na kuhakiki taarifa za anuani za makazi jumla ya milioni 2.3 huku taarifa mpya zaidi ya laki 5 katika halmashauri 28 zimeweza kukusanywa.
Hayo yameelezwa leo Aprili 16, 2024 jijini Dodoma na Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Bw. Mohamed Khamis Abdulla katika hafla ya kukabidhi vifaa na kuzindua majaribio ya kutoa huduma ya barua ya utambulisho wa mkazi kupitia mfumo wa kidijitali wa anuani za makazi (NaPA).
Amesema utekelezaji wa mfumo wa anwani za makazi ulianza mwaka 2010 na ulipangwa kukamilika ifikapo 2015 na kuanzisha mfumo wa anwani za makazi ni utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Posta ya mwaka 2003 hata hivyo makubaliano ya kikanda kupitia umoja wa Posta Afrika yaani Pan Africa Postal Union -PAPU makubaliano ya kimataifa kupitia Umoja wa Posta Duniani yaani Universal Postal Union - UPU na Ilani ya uchaguzi ya CCM ya miaka mitano, 2020 – 2025 hata hivyo mpango huo haukukamilika kwa wakati kutokana na kukosa jitihada za pamoja na ufinyu wa bajeti.
“Oparesheni Anwani za Makazi ilikuwa na mafanikio makubwa ambapo zaidi ya Anwani za Makazi milioni 12.3 zilisajiliwa na taarifa zake kuhifadhiwa kwenye Mfumo wa Anwani za Makazi unaojulikana kwa jina la NaPA kwa lugha rahisi, NAPA ni daftari la kidijitali la ukazi ambalo linawezesha serikali kuu, Serikali za mtaa au Shehia pamoja na mambo mengine kujua idadi wa watu walio kwenye eneo husika hivyo urahisi wa kupanga mipango mbalimbali ya maendeleo kwa kuzingatia uhalisia wa watu na huduma zilizopo katika eneo hilo.
Na kuongeza “Baada ya oparesheni ya anwani za makazi kukamilika, Wizara kwa kushirikiana na TAMISEMI (Kwa upande wa Tanzania bara), TAMISEMIM na Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi (Kwa upande wa Zanzibar), tumeendelea kusafisha na kuhuisha taarifa zilizokusanywa wakati wa oparesheni kwa ajili ya kuwa na taarifa sahihi kila wakati ili ziweze kuleta tija katika matumizi yake hivyo hadi sasa zaidi ya taarifa za Anwani Milioni 2.3 na kukusanywa taarifa mpya zaidi ya laki 5 katika halmashauri 28, hivyo Wizara kwa kushirikiana na TAMISEMI kwa upande wa Tanzania bara pamoja na TAMISEMIM na Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi (Kwa upande wa Zanzibar), imejipanga kuhakikisha uhakiki wa taarifa katika mikoa yote nchini unakamilika ifikapo Juni, 2025.
Bw. Abdulla amesema, majengo yalibandikwa vibao vya namba za nyumba pamoja na nguzo za majina ya barabara ziliwekwa kwenye mitaa hivyo wanatambua kwamba baadhi ya maeneo hayakuwekewa miundombinu hiyo lakini kupitia zoezi hili endelevu chini ya usimamizi wa halmashauri na serikali za mitaa.
Katika hatua nyingine Bw. Abdulla amesema pamoja na uhakiki uliofanyika, mkakati wa Wizara ni kuhakikisha kila mwananchi anakuwa na Anwani ya Makazi ambayo ataitumia katika kujitambulisha ili kufikia dhamira ambayo wamejipanga kujenga uwezo kwa watendaji wa Kata, Mitaa, vijiji na shehia kote nchini na akisema lengo ni kujenga timu kubwa ya wataalam wenye uwezo wa kutoa huduma za anwani za makazi kwa wananchi walio kwenye ngazi za msingi na hadi sasa na baada ya oparesheni ya anwani za makazi wataalam na watendaji 6,613 katika halmashauri 28 wamejengewa uwezo.
Na kuongeza kuwa “Lengo la wizara kwa upande mwingine ni kuhakikisha taarifa za Anwani za Makazi zilizosajiliwa kwenye mfumo wa NAPA zinatumika ili kufikia malengo yaliyokusudiwa, Huduma mbalimbali zinapatikana ikiwemo ya mwananchi kuweza kutambua kupitia mfumo wa NAPA huduma zote zinazopatikana eneo lolote la karibu akiwa sehemu yoyote nchini kama vile hospitali, hoteli, masoko, shule, maduka ya dawa, Vyuo, sehemu za kuabudi (Makanisa au misikiti) na huduma nyinginezo,” amesema Bw. abdulla.
Eneo lingine ambalo limekamilishwa ni kutengenezwa kwa moduli kwenye mfumo wa NAPA unaowezesha mwananchi kuomba barua ya utambulisho wa Mkazi bila hitaji la kwenda kwenye ofisi za serikali ya mtaa na kwa utaratibu wa sasa, barua hizo zinapatikana kwenye ofisi za watendaji ambapo mwombaji anatakiwa kufika katika ofisi husika ili kupatiwa barua hiyo kwani baadhi ya huduma zinahitaji mwananchi kuwasilisha barua ya kutambulisha ukaazi wake, baadhi ya huduma hizo ni pamoja na huduma za mikopo, huduma za pasipoti, baadhi ya maombi ya kazi kama za ulinzii, vitambulisho vya NIDA, uwekaji wa dhamana kwa watuhumiwa na hizio ni baadhi ya huduma kati ya nyingi zilzopo zinazohitaji barua ya utambulisho wa mkazi.
Kwa upande wa mwakilishi wa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI Rachel Kaduma amesema huduma hiyo inakwenda kufanyika katika maeneo ya ngazi za msingi ya kata, mitaa na vijiji ambayo inasimamia na TAMISEMI itahakikisha kila mtu anatimiza wajibu wake ili matarajio ya serikali yaweze kufikiwa na hatua hiyo ni utekelezaji wa zile R nne za Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hususani ile ya “Reforms” na kuongeza kupitia huduma hii wanakwenda kuleta mageuzi katika utoaji wa huduma ya upatikanaji wa barua za utambulisho pasipo kufika ofisi za ngazi za msingi.
Uzinduzi huo umeenda sambamba na ugawaji wa vitendea kazi ikiwemo kompyuta za mezani, printa na vishikwambi kwa watendaji walio katika maeneo ya majaribio hayo yatafanyika kwenye mitaa 13 ambapo mitaa 9 ni ya Tanzania bara na minne ya Zanzibar.
Uzinduzi wa leo ni wa upande wa Tanzania bara ambapo maandalizi ya uzinduzi kwa upande wa Zanzibar yatafanyika kwa tarehe itakayopangwa na yanataribiwa na Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi (Zanzibar) kwa kushirikiana na TAMISEMIM.
No comments:
Post a Comment