Rais wa Uganda Yoweri Museveni wa pili kulia na Rais wa China Xi Jinping wa pili kushoto walipokutana kwenye Ukumbi wa Great Hall of the People, Juni 25, 2019, Beijing. |
China imemwalika waziri wa nishati wa Uganda mjini Beijing kujadili kuhusu bomba la mafuta ghafi la dola bilioni 5 la nchi hiyo ofisi ya rais wa Uganda ilisema Ijumaa.
Maendeleo hayo yanaweza kuashiria mafanikio katika juhudi za Uganda kuwashawishi wafadhili wa China kufadhili bomba hilo, ambalo nchi hiyo inahitaji kuanza uzalishaji ghafi kutoka kwenye maeneo ya mafuta ambayo yaligunduliwa mwaka 2006.
Ufadhili unaowezekana wa China unachukuliwa kuwa muhimu baada ya benki za nchi za Magharibi kukataa kufadhili bomba hilo baada ya shinikizo kutoka kwa wanamazingira ambao walisema mradi huo utaongeza uzalishaji wa hewa chafu dunianiz.
No comments:
Post a Comment