Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) Mhe. Usekelege Nahshon Mpulla, amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) ofisi ya Tanzania Bi. Caroline Khamati Mugalla, katika ofisi za shirika hilo, tarehe 04 Aprili, 2024 jijini Dar es Salaam.
Mazungumzo hayo yalijikita katika kutekeleza Mikataba ya msingi ya Shirika la Kazi Duniani pamoja na mikataba mingine ambayo Tanzania imeiridhia, hususan katika masuala ya utatuzi bora wa migogoro ya kikazi Tanzania bara.
Aidha, mtendaji mkuu wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA), ameeleza utayari wa CMA katika kuhakikisha wanashirikiana na Shirika la Kazi Duniani katika kuimarisha ushirikiano baina ya taasisi hizi mbili, katika kusimamia mikataba ya kimataifa ya shirika hilo.
Mkurugenzi wa CMA aliambatana na Afisa Mfawidhi Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) Kinondoni, Dar es Salaam, ambaye pia ni Muamuzi mwandamizi, Mhe. Grace Wilbard Massawe
No comments:
Post a Comment