DKT. BITEKO AWATAKA WATANZANIA, WASIKUBALI KUGAWANYWA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, April 20, 2024

DKT. BITEKO AWATAKA WATANZANIA, WASIKUBALI KUGAWANYWA

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe, Dkt. Doto Biteko akiweka
jiwe la msingi la ujenzi wa kituo cha Afya Shehiya ya Kinyikani Jimbo
la Kojan wilaya ya Wete mkoa wa Kaskazini Pemba tarehe 20 Aprili 2024.
Wa kwanza kulia (mbele) ni Mbunge wa Jimbo la Kojani ambaye pia ni
Naibu Waziri wa Fedha wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Hamad
Chande
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe, Dkt. Doto Biteko
akizungumza mara baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa kituo
cha Afya Shehiya ya Kinyikani Jimbo la Kojan wilaya ya Wete mkoa wa
Kaskazini Pemba tarehe 20 Aprili 2024.

Na Mwandishi Wetu, Zanzibar 

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Biteko,
amewataka Watanzania katu wasikubali kugawanywa kwa namna yoyote na badala yake waulinde na kudumisha Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambao unatimiza miaka 60 ifikapo tarehe 26 Aprili, 2024 na serehe za
maadhimisho yake yatafanyika Jijini Dar es Salaam.


Dkt. Biteko amesema kuimarika kwa Muungano kumetokana na Amani,
utulivu na mshikamano miongoni mwa Watanzania na hivyo Muungano ni moja ya Tunu za Taifa ambao unahitaji kulindwa ili kuenzi matunda
yaliyopatikana.


Dkt. Biteko ameyasema hayo leo 20 Aprili 2024, mara baada ya kuweka
jiwe la Msingi la ujenzi wa Kituo cha Afya Shehiya ya Kinyikani Wilaya
ya Wete, Mkoa wa Kaskazini Pemba, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho
kuelekea miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.


"Tanzania ndio nchi pekee barani Afrika na Duniani kwa ujumla kuwa na Muungano imara na thabiti kwa miaka mingi, hivyo ni vema kuulinda kwa namna yoyote ile" Alisema Dkt. Biteko


Awali, Dkt. Biteko alipata fursa ya kukagua ujenzi wa kituo hicho cha
Afya cha Kinyikani, kinachojengwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii
nchini (TASAF) na kusimamiwa na wakala wa ujenzi Zanzibar ZBA, ambapo hadi kukamilika kwake kituo hicho kitagharimu shilingi milioni 500.


Pia amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.
Samia Suluhu Hassan na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi kwa kuhakikisha miradi ya maendeleo zikiwemo Zahanati, Vituo vya Afya, Shule na Miundombinu mbalimbali
inatekelezwa.


Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Waziri wa nchi Afisi ya makamu wa
pili wa Rais Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi Mhe. Hamza Hassan
Juma, amepongeza jitihada zinazofanywa na Rais Dkt. Hussein Ali Mwinyi kwa kuwaletea wananchi maendeleo na kuhakikisha huduma za Afya
zinaimarika kisiwani Pemba.


Kwa upande wake Naibu Waziri wa Fedha ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kojani Mhe. Hamad Chande, amewashukuru wananchi wa Jimbo la Kojani kwa kuchangia Takriban asilimia 10 ya ujenzi wa kituo hicho cha Afya
pamoja na nguvu kazi kwenye ujenzi wa kituo hicho, na kuwaahidi pindi
ujenzi utakapokamilika atatoa gari la jipya la wagonjwa ili kurahisha
huduma kwa wakazi wa maeneo hayo.


Kituo hicho cha afya kitakuwa na huduma mbalimbali ikiwemo huduma za wagonjwa wa Nje OPD, Huduma za Uzazi Mama na Mtoto, Huduma za Maabara,Ultra Sound, Pamoja na huduma nyingine za tiba.


Hafla hiyo imehudhuriwa na Waziri wa nchi Afisi ya Makamu wa pili wa
Rais Sera, Uratibu na Baraza la wawakilishi Mhe. Hamza Hassan Juma, pamoja na viongozi wengine na wawakilishi wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF, Maadhimisho ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yatafikia kilele chake tarehe 26 Aprili, 2024 katika sherehe za Kitaifa zitakazofanyika Jijini Dar Es Salaam.


Kituo hicho cha afya kitakuwa na huduma mbalimbali ikiwemo huduma za wagonjwa wa nje yaani OPD, huduma ya mama na mtoto, huduma za maabara, ultra sound, chanjo pamoja na huduma za kujifungua.


Hafla hiyo imehudhuriwa na Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Wenyeviti wa CCM Wilaya, Wawakilishi wa Shehiya mbalimbali na wananchi wa Kinyikani.

No comments:

Post a Comment