JE, MZOZO KATI YA ISRAEL NA IRAN UNAWEZA KUSABABISHA VITA VYA TATU VYA DUNIA? - GAZETI LA THE INDEPENDENT. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Friday, April 19, 2024

JE, MZOZO KATI YA ISRAEL NA IRAN UNAWEZA KUSABABISHA VITA VYA TATU VYA DUNIA? - GAZETI LA THE INDEPENDENT.



Tunaanza ziara ya magazeti ya leo na gazeti la The Independent la Uingereza, ambalo lilihoji ni kwa kiasi gani mwelekeo wa mzozo wa sasa kati ya Israel na Iran unaweza kupanuka na kugeuka kuwa vita vya tatu vya dunia.


Mtaalamu wa masuala ya Mashariki ya Kati, David B. Roberts, alielezea hofu yake juu ya uwezekano wa vita vya kikanda kugeuka kuwa kitu kikubwa zaidi, kinachohitaji kuingilia kati kwa nguvu za kikanda pamoja na nchi za nje ya ukanda kama vile Marekani na Uingereza.


Amesisitiza kuwa, Tehran ilitoa onyo la kutosha kwa Israel na Marekani kuhusu mpango huo, na kuruhusu muungano wa dharura kujiandaa kwa mashambulizi yanayokaribia, na Tehran haikuiomba Hizbullah kutumia makombora yake 150,000.


Mwandishi anasema kwamba uongozi wa Iran ulitaka kulipiza kisasi dhidi ya Israeli, lakini bila kupiga pigo kubwa kwa kiwango ambacho kingesababisha kisasi kikubwa cha Israeli na labda ushiriki wa Marekani.






Wasiwasi unaongezeka sana kuhusiana na hali ambapo Israel inalenga mpango wa nyuklia wa Iran.


Lakini Israel haiwezi kuanzisha operesheni hiyo peke yake, na ingehitaji vikosi vya Marekani vilivyoko katika Ghuba kusaidia, na utawala wa Marekani hadi sasa umekataa kujiunga na operesheni yoyote kama hiyo.


Mwandishi anaamini kuwa Israel inaweza kutia chumvi majibu yake, na kulipiza kisasi kutaenea sana hivi kwamba viongozi wa Iran watahisi kulazimishwa kujibu, "jambo ambalo litaimarisha hofu ya mzozo mkubwa."


Iwapo Iran itafanyiwa mashambulizi makubwa na Israel, duru ijayo ya kulipiza kisasi kwa Iran itajumuisha kwa hakika Hezbollah kushambulia kaskazini mwa Israel.


Anaongeza kuwa upanuzi huo wa mzozo hautasalia katika eneo la Levant, na ikiwa vikosi vya kijeshi vya Magharibi vitajaribu kuiunga mkono Israel, vitalengwa waziwazi huku wakilinda anga dhidi ya makombora na ndege zisizo na rubani za Iran.


Athari za kiuchumi za kijiografia za mzozo unaoendelea na wa mara kwa mara katika Mashariki ya Kati zinaweza kusababisha bei ya mafuta kupanda, na hatua ngumu za za kuufufua uchumi duniani kote.

No comments:

Post a Comment