Imeelezwa kuwa licha ya kampeini mbalimbali ambazo zimekuwa zikifanywa na serikali hususani jeshi la polisi za kukabiliana na vitendo vya ukatili lakini ndani ya Mkoa wa Dodoma vitendo hivyo bado vipo juu.
Hayo yameelezwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Theopista Mallya leo Aprili 12, 2024 jijini Dodoma ,wakati akizindua kampeni maalumu ya kukabiliana na vitendo hivyo inayokwenda kwa jina la "FAMILIA YANGU HAINA MHALIFU" ambapo uzinduzi huo umefanyika katika shule ya Msingi Chaduru iliyopo jijini Dodoma.
Aidha SACP Mallya amezungumzia kuhusu hali ya usalama katika Mkoa wa Dodoma ambapo amesema kuwa kwa sasa hali iko sawa licha ya taarifa za chini chini kuripoti kuwa eneo la Kikuyu bado uhalifu upo.
"Tutaongeza uangalizi eneo linaloitwa Kikuyu ambapo bado taarifa zinaonesha kuna uhalifu ila kuna wale watu wanawahi stand asubuhi bodaboda wamekuwa wanawavizia na kuwanyang'anya simu na vitu vingine hapo napo tutaongeza uangalizi ili kuhakikisha Dodoma inakuwa shwari," ameeleza SACP Mallya
Kwa upande wake Afisa Elimu Kata ya Makole Mwalimu Aneth Fredrick amesema unzishwaji wa kampeini hiyo kutaenda kuwasaidia kwenye malezi hususani katika kipindi hiki ambacho maadlil yanaonekana kushuka zaidi na watoto ndiyo waliothirika zaidi.
Nao baadhi ya wanafunzi waliohudhuria katika uzinduzi huo wamesema kuwa kampeini hiyo itaenda kuwa na mchango mkubwa hususani katika kukabiliana na uharifu pamoja na unyanyasaji unaofanyika majumbani.
No comments:
Post a Comment