Mtu mmoja akiwa amebeba bango la TikTok mbele ya mahakama ambapo kesi ya Donald Trump ilianza kusikilizwa Aprili 15, 2024, huko New York. |
Kampuni ya Tiktok siku ya Jumapili ilitoa wasi wasi wake juu ya masuala ya uhuru wa kujieleza kuhusiana na muswaada uliopitishwa na baraza la wawakilishi wa Marekani ambao unataka kuupiga marufuku.
Bunge lilipitisha sheria hiyo siku ya Jumamosi kwa tofauti ya kura 360 kwa 58 ambapo sasa unahamia kwenye baraza la Seneti ambapo unaweza kupigiwa kura katika siku zijazo.
Rais Joe Biden hapo awali alisema atatia saini sheria hiyo.
Hatua ya kujumuisha TikTok katika msaada mkubwa wa usaidizi wa mambo ya nje inaweza kusukuma kwa haraka ratiba ya marufuku inayoweza kutokea baada ya muswaada tofauti wa awali kukwama katika baraza la Seneti la Marekani.
Bunge limepitisha sheria hiyo ya kupiga marufuku TikTok nchini Marekani ikiwa mmiliki wake mwenye makao yake China hatauza hisa zake, na kutuma muswaada kwenye baraza la Seneti kama sehemu ya muswaada mkubwa zaidi ambao unajumuisha msaada kwa Ukraine na Israel.
No comments:
Post a Comment