Ferdinand Shayo ,Manyara .
Mamia ya Wafanyakazi wa Kampuni ya kuzalisha vinywaji changamshi ya Mati Super Brands Limited wameshiriki maadhimisho ya siku ya Wafanyakazi ya Mei Mosi yaliyofanyika kimkoa Katika Viwanja vya Tanzanite Kwaraa Wilayani Babati Mkoani Manyara na kupambwa na msafara mrefu wa magari ya kusambaza vinywaji kutoka kwenye kampuni hiyo.
Mkurugenzi wa Kamapuni hiyo David Mulokozi amesema kuwa maonyesho hayo ya magari yaliyotanguliwa na farasi yanalenga kuonyesha ukubwa wa kampuni hiyo katika kusambaza bidhaa zake za Strong Dry Gin,Tanzanite Premium Vodka na Sed Pineapple flavoured gin.
Mulokozi amesema kuwa kampuni hiyo itaendelea kuwahakikishia wafanyakazi wake Maslahi bora ili waweze kufanya kazi kwa bidii na kuzingatia weledi.
Mkuu wa Wilaya ya Babati Lazaro Twange amesema kuwa serikali itaendelea kuweka mazingira rafiki kwa wafanya kazi ili waweze kutimiza majukumu yao na kuleta tija mahali pa kazi.
Twange amepongeza serikali pamoja na sekta binafsi kwa kuwa mstari wa mbele kuajiri na kupunguza changamoto ya ajira nchini.
No comments:
Post a Comment