MCHEZAJI WA KAIZER CHIEFS AFRIKA KUSINI AUAWA KWA KUPIGWA RISASI. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, April 4, 2024

MCHEZAJI WA KAIZER CHIEFS AFRIKA KUSINI AUAWA KWA KUPIGWA RISASI.


Mwanasoka wa Afrika Kusini Luke Fleurs ameuawa kwa kupigwa risasi katika utekaji nyara wa gari, timu yake inasema. 


Ufyatuaji huo ulifanyika katika kituo cha mafuta usiku wa kuamkia leo katika kitongoji cha Johannesburg, Florida. 


Kijana huyo mwenye umri wa miaka 24 alikuwa akisubiri kuhudumiwa alipofikiwa na watu wasiojulikana wenye silaha, ambao walimwamuru ashuke nje ya gari. 


Mmoja wa washukiwa alikimbia eneo la tukio na gari la Fleurs baada ya kumpiga risasi. 


"Washukiwa walimnyooshea bunduki na kumtoa nje ya gari lake, kisha wakampiga risasi moja kwenye sehemu ya juu ya mwili," msemaji wa polisi wa Gauteng Luteni Kanali Mavela Masondo aliambia vyombo vya habari vya ndani. 


Timu yake, Kaizer Chiefs, inasema kifo hicho kilikuwa "cha kusikitisha". Ilisema polisi wanashughulikia suala hilo na taarifa zaidi zitawasilishwa kwa wakati unaofaa. 


Beki Fleurs alijiunga na Kaiser Chiefs mwaka jana. 


Hapo awali alichezea SuperSport United. Katika tovuti yake, Kaiser Chiefs inaeleza Fleurs kama "beki wa kiwango cha juu" na "uwezo mkubwa wa kiufundi". 


Alianza kazi yake mnamo 2013 katika Chuo cha Ubuntu Cape Town, kulingana na vyombo vya habari vya ndani. 


Mashabiki wa soka wamejitokeza kwenye mitandao ya kijamii kumuomboleza.

No comments:

Post a Comment