Bondia namba moja Tanzania, Hassan Mwakinyo
'Champez' amewajia juu wanaomkashifu bondia
mkongwe, Abdallah Pazi maarufu kama Dullah Mbabe aliyepoteza pambano lake Kwa knock out (K.O) dhidi ya bondia muingereza Callum Simpson kwenye round ya 4 katika pambano la raundi 10.
"Leo hii watu wengi bila kujua mtu kama Dullah Mbabe ni kwa namna gani? Hautaacha kuzungumzia mchango wake mkubwa kwenye tasnia yetu ya ngumi na katika mema yake aliwahi kushinda nje ya nchi mara mbili kwa kupiga watu KO tena nchi ngumu kama Russia, jambo ambalo kwa viwango vya wachezaji wetu hutokea kwa nadra na bahati mbaya sana tena kutoka karne moja mpaka karne nyengine.
"Wakati huo hakuna aliekuwa proudly na ushindi wake wala kuzungumzia popote pale kama ambavyo leo naona machafuko ya kila aina matusi na kashfa za watu juu yake kuona kama kukosa matokeo kwake ni sehemu ya kufurahisha wengine.
"Anyway pole sana msena wangu wewe ni katika watu naujua mchango wako mkubwa sana kwenye
maendeleo ya hatua zangu na bado hakuna siku itafika nikutoe thamani na heshima yako.
"Kibinaadam niseme kwamba ni Mwenyezi Mungu
pekee ndio anajua ni kwa nini anakupitisha kwenye
haya usikate tamaa kaka hakuna namna utafanikiwa kwa kuepuka maumivu utakayo lazimika kupitia.
Achana na mihadarat na makundi ya ajabu fanya kazi," amesema Mwakinyo.
No comments:
Post a Comment