MIRADI NANE YA MAENDELEO YENYE THAMANI YA ZAIDI YA BILLION 3.6 INATARAJIWA KUZINDULIWA NA MBIO ZA MWENGE 08 APRIL 2024 WILAYA YA SAME MKOANI KILIMANJARO. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Sunday, April 7, 2024

MIRADI NANE YA MAENDELEO YENYE THAMANI YA ZAIDI YA BILLION 3.6 INATARAJIWA KUZINDULIWA NA MBIO ZA MWENGE 08 APRIL 2024 WILAYA YA SAME MKOANI KILIMANJARO.



Na Ashrack Miraji, Same Kilimanjaro.


Mkuu wa Wilaya ya Same Kasilda Mgeni amesema jumla ya miradi nane 08 ya maendeleo yenye thamani ya zaidi ya shilingi Bilioni 3.6 inatarajiwa kupitiwa na mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2024 ikiwemo barabara, vijana, elimu, maji, afya pamoja na mazingira.


Akizungumza na mwandishi wetu ofisin kwake leo mkuu wa Wilaya amebainisha hayo wakati akitoa taarifa ya mapokezi ya Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2024 ambao utapokelewa kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Njoro Aprili 08 asubuhi ukiwa unatokea halmashauri ya Wilaya ya Mwanga.


Aidha DC Mgeni amesema baada ya kupokea Mwenge utakimbizwa Wilayani humo Kilometa 138.4 na katika mbio hizo miradi minne itafunguliwa, mitatu itatembelewa na mmoja utawekewa jiwe la msingi ambalo ni mradi wa kwanza wa barabara uliopo Same Mjini.


“Niwaombe wananchi wote ambao wapo Wilayani Same wahakikishe wanajitokeza kwa wingi katika Shule ya Msingi Njoro kuupokea Mwenge wa Uhuru kwa shamla shamla, nderemo na vifijo lakini pia kujitokeza kwa wingi kwenye mkesha wake pale uwanja wa Shule ya Msingi Hedaru.”


Pia amesema kuwa maandalizi muhimu ya kuupokea Mwenge huo tayari yamekamilika ikiwemo miradi ya maendeleo itakayopitiwa lakini pia jukwaa la viongozi pamoja na la wasanii kwenye eneo la mkesha wa Mwenge ambapo imepangwa kufanyika katika viwanja vya Shule ya Msingi Hedaru.


Nao baadhi ya viongozi wa madhehebu ya dini Wilayani humo wakizungumza kwa nyakati tofauti tofauti wamesema kuwa wananchi wanapaswa kutambua kufika kwa Mwenge wilayani humo ni moja ya sehemu ya maendeleo kwao kwani miradi mbali mbali ya maendeleo itafunguliwa hivyo hawanabudi kujitokeza kwa wingi kusikiliza maelekezo muhimu kutoka kwa viongozi wa mbio za Mwenge kitaifa.


Kwa mwaka 2024 mbio za Mwenge wa Uhuru zimebeba kaulimbiu isemayo “Tunza Mazingira na Shiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa Ujenzi wa Taifa Endelevu”.




No comments:

Post a Comment