Fanyeni kazi achaneni na mawazo potofu ya kuwaza imani za kishirikina katika baishara, mnaangamia kwa kukosa maarifa, kwa kuendekeza vitendo vya imani za kishirikina vinavyopelekea kufanya ukatili na mauaji.
Kauli hiyo imetolewa April 25, 2024 na Kamanda wa Polisi Mkoa Wa Dodoma Kamishna Msaidizi Wa Polisi (SACP) Theopista Mallya wakati akizungumza na wafanya biashara takribani 1000 wa soko la Majengo Jijini Dodoma ambapo pia aliulizwa maswali na kuyajibu kwa kuyatolea ufafanuzi.
Mallya amekemea vitendo vinavyofanywa na baaadhi ya wafanya biashara kuamini zaidi katika imani za kishirikina na kufanya vitendo vya kihalifu kama mauaji katika familia ili kupata mali na kukuza biashara.
Kamanda Mallya amewataka pia Wafanya bishara ya kuunza nyama katika mabucha kuepuka kuuza nyama ambazo ni haramu ambayo ni mifugo iliyoibiwa na kuuzwa bila kufuata utaratubu wa kisheria.
"Ng'ombe nyingi ni za wizi mtu anaibiwa mifugo, watu wanachinjia katika mapori wanabeba kwenye ndoo mnauzia wananchi vitu haramu; Nunua Ng,'ombe lipa kodi uza nyama kihalali" Amesema Mallya.
Aidha Mallya amewaasa wafanya biashara hao ambao ni wazazi na walezi kutotumia muda mwingi katika shughuli za baishara na kusau malezi kwa watoto kwa kuwakagua mara kwa mara pamoja na kuwakataza kucheza katika madimbwi ya maji hususani kipindi hiki mvua zinapo nyesha.
Katika Hatua nyengine Kamanda Mallya amefika katika kituo kipya cha Polisi kilichopo Mtumba na kufanya ukaguzi na kuangalia hatua za mwisho za ukamilishwaji wa kituo hicho na kuangalia huduma zinazoendelea kutolewa kwa wananchi.
Toka Dawati la Habari Polisi Dodoma
No comments:
Post a Comment