MTOTO WA LEBRON JAMES, ATANGAZA KUSHIRIKI KATIKA USAJILI WA NBA 2024. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, April 6, 2024

MTOTO WA LEBRON JAMES, ATANGAZA KUSHIRIKI KATIKA USAJILI WA NBA 2024.

Bronny James, mtoto mkubwa kati ya watoto watatu wa LeBron James.

Bronny James, mwana wa kiume wa mchezaji mashuhuri wa ligi ya mpira wa vikapu Marekani NBA ametangaza kwamba atajisajili katika uteuzi wa mwaka wa 2024 wa ligi hiyo yaani (2024 NBA draft).


Tangazo hili linajiri wakati ambapo kijana huyo mwenye umri wa miaka 19 alipatwa na mshtuko wa moyo akiwa mazoezini katika chuo kikuu cha Southern California (USC).


Alifanyiwa upasuaji wa moyo na kurejea chuoni kushiriki katika msimu wa ligi ya mpira wa vikapu ya vyuo vikuu Marekani katika mechi yake ya kwanza kama mchezaji mwezi Desemba.


Lebron ambaye anaongoza orodha ya wafungaji vikapu vingi zaidi katika michuano ya ligi ya NBA, hajaficha au kulifanya siri azimio lake la kutamani mwananwe kuche za naye mechi rasmi.


James mwenye umri wa miaka 39, ambaye anachezea timu ya Los Angeles Lakers, aliiambia kituo cha Habari cha ESPN 2o23 kwamba: ‘ Ninahitaji kucheza pamoja na mwanangu, nina hamu ya kuwa na Bronny uwanjani.’


Bronny alisema kwenye mtandao wake wa kijamii wa Instagram kwamba:  “Nimeshuhudia hali ngumu katika mwaka uliopita, lakini hayo yote yamenipa mafunzo na motisha ya kukuwa kama mwanamume, mwanariadha na mwanafunzi.”


Aliongeza kuwa “Nimefanya uamuzi wa kujisajili katika uteuzi huu wa NBA d huku nikiendelea kuchezea timu yangu ya chuoni, na pia nitajisajilia katika eneo la kutaka uhamisho wa NCCAA.”

No comments:

Post a Comment