Elad Katzir alitekwa nyara kutoka kusini mwa Israel tarehe 7 Oktoba. |
Jeshi la Israel limesema limepata mwili wa mwanamume aliyeketwa nyara na kuzuiliwa ndani ya Gaza, katika operesheni ya uvamizi wa kijeshi mjini wa Khan Younis.
Elad Katzir alitekwa kutoka mji wa Kibbutz Nir Oz wakati wa shambulizi ya kundi la Hamas kwenye eneo la kusini mwa Israel Oktoba 7.
Kwa mujibu wa jeshi la Israel na Mamlaka ya usalama nchini humo ISA, mwili wake umepatikana ndani ya Gaza katika opereshi ya usiku kucha na kurejeshwa Israel.
Alitambuliwa na wahudumu wa matibabu na familia yake imeaarfiwa.
IDF na ISA zimesema katika taarifa ya pamoja, kwamba: Mwili wa mateka Elad Katzir ambaye kulingana na taarifa za kijasusi, aliuawa akiwa amezuiliwa na kundi la kigaidi la Islamic Jihad, uliokolewa usiku kutoka Khan Younis na kurejeshwa katika himaya ya Israel.
Wamesema kwamba mwili huo ulitambuliwa kwa kutumia taarifa za kina za kijasusi.
Bwana Katzir mwenye umri wa miaka 47, alitekwa kutoka Niir Oz kwa Pamoja na mama yake Hanna mwenye umri wa miaka 77.
Mama yake aliachiliwa huru mwezi Novemba 2023, huku babake Avraham akiuawa katika eneo la Kibbutz, kulingana na IDA na ISA.
No comments:
Post a Comment