IKIWA bado siku moja kuelekea maadhimisho ya miaka 60 ya Muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) imesaini mkataba wa makubaliano (MOU) na Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma ya Zanzibar ( ZPPDA) kwaajili ya kushirikiana kujenga uzoefu kwa watendaji na kukuza maarifa ya kiutendaji kwa kubadilishana utaalam katika ununuzi wa umma.
Akizungumza mara baada ya kutiliana saini leo Aprili 25, 2024 jijini Dodoma Mkurugenzi Mkuu wa PPRA Eliakim Maswi amesema mara baada ya kusaini hati ya makubaliano hayo ya pande hizo mbili zitashirikiana katika kujenga uzoefu wa utendaji wao na kukuza taarifa ya kiutendaji.
"Tutafanya mambo yafuatayo Kubadilishana utaalamu katika kutekeleza mbinu za kimkakati na taaluma ya ununuzi na uondoaji wa Mali za umma, kushirikiana katika kuzitambua sheria,miongozo na taratibu ambazo zinaleta tija na uwajibikaji zinazoweza kupelekea matokeo chanya katika shughuli za ununuzi na uondoaji wa mali za umma,
"Kubadilishana taarifa na ujuzi muhimu unaohusu ununuzi na uondoaji wa Mali za umma ambao unaweza kuwa na manufaa kwa na mpaka hizo katika utendaji wa kazi zao, kuhabarishana,kupeana uzoefu na kuhusishana katika fursa za ushiriki katika majukwaa na mikutano ihusuyo Ununuzi wa Umma ya Kitaifa,Kikanda na Kimataifa"amesema.
Amesema pia makubaliano hayo ni katika kutengeneza ushirikiano maalum katika shughuli za ufuatiliaji,ukaguzi na uchunguzi unaojumuisha uchunguzi wa kuzingatia ni wa sheria na thamani ya fedha.
"Pia kushauriana kuhusu nyenzo za kisasa za utendaji wa majukumu ya Mamlaka zikiwemo mifumo ya Kielektroniki na vifaa vingine vya kisasa vya kazi za ukaguzi,uchunguzi na ufuatiliaji"amesema
Katika hatua nyingine Mkurugenzi Mkuu huyo amesema ili kukuza, kuboresha na kuendeleza uhusiano kwa mujibu wa makubaliano haya mamlaka zitashirikiana kufanya shughuli na vikao vya pamoja ambao sita kuwa ni jukumu la pamoja kuweka ratiba ya kila mwaka ya vikao vya pamoja vya ngazi zote,kuanzia Bodi za ,Menejimenti na Idara.
Amesema kila upande utakuwa na wajibu wa kuizingatia, kuifuata na kutekeleza ratiba hiyo pia Mtendaji au Idara ya upande wowote itakuwa na wajibu wa kutekeleza maazimio na maelekezo yanayotokana na vikao hivyo,pia ni wajibu wa muhusika kuwasilisha ripoti ya kutekeleza ni wa maelekezo,maazimio na maagizo hayo.
Aidha akizungumzia ukaguzi wa changamoto Maswi amesema kwa kuongozwa na mipaka ,ukomo na upeo wa ushirikiano kwa mujibu wa makubaliano pande zinazohusika zitashirikiana katika ukaguzi wa changamoto zinazozikabili katika utendaji wa shughuli zao kwa kubadilishana watendaji kwa muda utakaofikiwa kwa lengo la kujifunza na kubadilishana uzoefu na pia kutatua changamoto zinazozikabili mamlaka hizi.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji ZPPDA Othaman Juma Othman amesema kuwa matokeo ya ma Shirika hayo ni tunu ya Muungano iliyoachwa na waasisi wa Muungano kwani maono yao yamepelekea uongozi uliopo kuendelea kusisitiza taasisi kuwa na mashirikiano kwa kufanya kazi kwa pamoja kwa maslahi ya watanzania.
"Ilikuwa ni kona kutoka huku kwenda huku mpaka leo tunasaini MOU kuna kila sababu ya kuwashukuru Idara ya mwana sheria Mkuu wa Serikali pamoja na Wataalam wetu waliotayarisha kwani wamefanya kazi nzuri kwa kukutana mpaka kufikia leo"amesema
No comments:
Post a Comment