"Ni kweli kabisa kuwa maendeleo yamekuwa kwa kasi sana ila bado watanzania wenye bima za afya ni wachache sana ni asilimia 8 tu sasa idadi iliyobaki hawana bima kwa haraka tunaweza kusema hawana uhakika wa matibabu hivyo ili kuwa na uhakika wa matibabu bunge limepitisha sheria ya Bima ya Afya kwa wote itakayomhakikishia kila mwananchi kupata bima ya afya," amesema Prof. Kitila
Kuhusu hali ya ukuaji wa uchumi Prof.Kitila amesema kwa miaka 20 mfululizo uchumi umekua ukikua kwa asilimia 6 hadi 7.
Prof. Kitila amesema licha ya kuyumba kwa ukuaji wa uchumi mwaka 2020 hadi 2021 hadi asilimia 1 mpaka 4 kwa sababu ya UVIKO 19 lakini kwa mapambano yanayoendelea hivi sasa ukuaji wa uchumi umefikia asilimia 5.2
Amesema pia kumekuwa na ongezeko la mtandao wa Barabara za zege na lami zinazounganisha mikoa kutoka kilomita 4179 mwaka 2000 hadi kufikia kilomita 11,966 mwaka 2022.
No comments:
Post a Comment