SARATANI YA MLANGO WA SHINGO YA KIZAZI HUKATIZA MAISHA YA WANAWAKE MILIONI 6 KILA MWAKA AFRIKA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Friday, April 12, 2024

SARATANI YA MLANGO WA SHINGO YA KIZAZI HUKATIZA MAISHA YA WANAWAKE MILIONI 6 KILA MWAKA AFRIKA


Na Okuly Julius Dodoma

Takwimu zinaonesha kila mwaka yanapatikana maambukizi mapya ya ugonjwa wa saratani ya Mlango wa Kizazi kwa wanawake zaidi ya Milioni 10, huku wanaopoteza maisha ni zaidi ya Milioni 6 Barani Afrika kila mwaka.

Hayo yameelezwa na Afisa Mpango wa Taifa wa chanjo Lotalis Gadau kutoka Wizara ya Afya wakati akitoa mafunzo kwa waandishi wa habari kuhusu chanjo ya saratani ya mlango wa shingo ya kizazi (HPV) kuelekea maadhimisho ya Wiki ya chanjo ambayo itaanza Aprili 22 hadi 28 mwaka huu.

Kutokana na hilo Gadau amebainisha kuwa Tanzania ni nchi ya Tatu kwa kuwa na idadi kubwa ya Wagonjwa wa Saratani ya Mlango wa kizazi katika Bara la Afrika.

Pamoja na hayo amesema kuwa wagonjwa wengi takribani 70% wamekuwa wakifika katika Vituo vya Afya wakiwa na hali mbaya na kutoa wito kwa jamii kuhakikisha wanakuwa na utaraibu wakupima Mara kwa mara ili kuwa salama.

Akielezea kuhusu Chanjo ya Saratani ya Mlango wa shingo ya kizazi amesema Chanjo hiyo ni salama na ni dozi ya Mara moja na inatolewa tofauti na awali ilikuwa inatolewa kwa awamu mbili ambapo wanaopatiwa chanjo hiyo ni watoto wakike kuanzia umri wa miaka 9 hadi 14.

Ni muhimu sasa kwa wazazi kuhakikisha wanawahamasiha Watoto wao kujitokeza kupata Chanjo hiyo ya HPV ili kuwalinda na maambukizi ya ugonjwa huo.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Idara ya Kinga,Wizara ya Afya,Dk.Tumaini Haonga amesema kutokana na ugonjwa kuwa na Kinga Serikali imeamua kuna na Mpango wa kutoa Chanjo hiyo kwa Watoto na mabinti ili kupambana na ugonjwa huo.

No comments:

Post a Comment