NAIBU WAZIRI AYOUB ASHIRIKI MKUTANO WA TUME YA PAMOJA YA USHIRIKIANO TANZANIA NA UGANDA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, March 14, 2026

NAIBU WAZIRI AYOUB ASHIRIKI MKUTANO WA TUME YA PAMOJA YA USHIRIKIANO TANZANIA NA UGANDA


Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud, ameshiriki katika Mkutano wa Tano wa Tume ya Pamoja ya Ushirikiano (Joint Permanent Commission - JPC) kati ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Uganda uliofanyika kwa lengo la kuimarisha ushirikiano wa pande mbili katika sekta mbalimbali za maendeleo.

Katika mkutano huo uliofanyika Machi 13, 2026 jijini Dar es Salaam, wajumbe wamejadili masuala mbalimbali ikiwemo mashirikiano ya kidiplomasia na kisiasa, masuala ya ulinzi na usalama pamoja na uhamiaji.

Kadhalika, Viongozi hao wamejadili maendeleo ya miundombinu ikiwemo sekta za ujenzi, usafirishaji na nishati ambazo ni muhimu katika kukuza uchumi na kurahisisha biashara kati ya Tanzania na Uganda.

Vilevile, wamejadiliana namna vitambulisho vya Uraia vya Tanzania na Uganda vinaweza kutumika kama nyaraka rasmi vya utambulisho wakati wa kusafiri kati ya nchi hizo mbili. Lengo la hatua hii ni kuhakikisha kwamba vitambulisho vya taifa vinavyotolewa na pande zote mbili vinatambulika pamoja na kuwarahisishia wananchi wa nchi hizo mbili kusafiri kwa urahisi zaidi

Kikao hicho ni hatua muhimu katika kuimarisha ushirikiano wa muda mrefu kati ya Tanzania na Uganda, pamoja na kuendeleza mahusiano ya kirafiki na kidiplomasia kwa manufaa ya wananchi wa nchi hizo mbili.



No comments:

Post a Comment