Na Okuly Julius , Dodoma
Ameyasema hayo leo Aprili 15,2024 jijini Dodoma, wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya mafanikio ya miaka 60 ya Muungano wa Tanzania kwa ofisi hiyo ya Rais. Ambapo Utaratibu huu unatekelezwa kwa mujibu wa Waraka wa Serikali wa tarehe 10 Mei, 2013
Pia Mh.Simbachawene ameongeza kuwa kutokana na kukua kwa teknolojia, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma imejenga program ya rununu (Ajira Portal Mobile App) inayopatikana kwenye PlayStore na ApStore za simu janja ili kuwarahisishia waombaji fursa za ajira kupata taarifa za uwepo wa fursa za ajira kiganjani mwao.
"Ili kuwafikia wadau na walengwa wa ajira kwa haraka na gharama nafuu, katika kipindi hiki cha miaka 60, ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, imejenga mfumo wa kidijitali wa ajira Serikalini ujulikanao kwa jina la Ajira Portal- https://portal.ajira.go.tz."amesema Simbachawene
Amesema katika kipindi hicho cha miaka 60 ya Muungano, Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma imekuwa ikifanya kazi na Tume ya Utumishi wa Umma Zanzibar inayoratibu masuala ya ajira kwa watumishi wa umma ili kurahisisha zoezi la kutangaza nafasi za kazi na kuwafikia waombaji walio wengi kwa uharaka zaidi.
"Katika kuimarisha zaidi muungano wetu, wataalam wa rasilimaliwatu hasa wanaojihusisha na masuala ya ajira kwa nyakati mbalimbali, wamekuwa wakibadilishana uzoefu. Ushirikiano huu, umekuwa chachu ya kuendelea kudumisha muungano wetu kwa kupata watumishi wenye sifa na weledi wa kutosha," ameeleza Simbachawene
Katika hatua nyingine Mh. Simbachawene ameelezea mafanikio Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) kwa Awamu ya Tatu kwa sasa inatekeleza Kipindi cha Pili cha Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini ambacho kinafanyika katika Mamlaka ya maeneo ya utekelezaji 186 ya Tanzania Bara na Zanzibar yakihusisha Halmashauri za Wilaya, Miji, Manispaa na Majiji ya Tanzania Bara na Unguja na Pemba kwa upande wa Zanzibar.
Amesme lengo ni kuziwezesha Kaya za Walengwa kutumia fursa za kuongeza kipato, kutumia huduma za Kijamii na Kiuchumi na kuwekeza katika kujenga na kuendeleza watoto wao ambao ni rasilimaliwatu.
"Katika kipindi cha miaka 60 ya Muungano, mpango huu umekuwa na manufaa makubwa mathalani katika eneo la Uhawilishaji wa Ruzuku kwa Walengwa ambapo kiasi cha Shilingi bilioni 824.4 kililipwa kwa Kaya Maskini 1,321,098 Tanzania Bara na Shilingi bilioni 41.2 ililipwa kwa Kaya Maskini 50,818 Zanzibar ili kuziwezesha kumudu gharama za msingi za maisha na kupeleka watoto wao shule na Kliniki," ameeleza Simbachawene
Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma nayo inatimiza miaka kumi na mitano (15) tangu kuanzishwa kwake Mwaka 2009.
No comments:
Post a Comment