Rais Emmanuel Macron amesema kuwa Ufaransa na nchi nyingine zingeweza kukomesha mauaji ya halaiki ya Rwanda mwaka 1994, ambapo Wahutu wenye msimamo mkali waliwaua zaidi ya Watutsi 800,000 na Wahutu wenye msimamo wa wastani.
"Ufaransa, ambayo ingeweza kukomesha mauaji ya halaiki na washirika wake wa Magharibi na Afrika, haikuwa na nia ya kufanya hivyo," Bw Macron alisema katika ujumbe wake wa video.
Video hiyo inatazamiwa kuoneshwa wakati wa ukumbusho wa 30 wa mauaji ya halaiki ya Rwanda siku ya Jumapili, ofisi ya Rais Macron ilisema.
Hafla hiyo inatazamiwa kuhudhuriwa na wageni kadhaa wa kimataifa akiwemo Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa Stéphane Séjourné na Rais wa zamani wa Marekani Bill Clinton.
Uhusiano kati ya Ufaransa na Rwanda hivi karibuni umekuwa mzuri, kufuatia miaka mingi ya mvutano kuhusu madai ya Ufaransa kuhusika katika mauaji ya halaiki.
Ufaransa imeshutumiwa kwa kushindwa kuchukua hatua za kutosha kukomesha mauaji ya kimbari ya Rwanda.
Viongozi wa Ufaransa wamekanusha kuhusika katika mauaji hayo ya kimbari.
Hata hivyo, katika ziara yake nchini Rwanda mwaka wa 2021, Bw Macron alisema kwamba Ufaransa ilikuwa na wajibu wa "kutambua mateso ambayo imewasababishia watu wa Rwanda kwa kuthamini ukimya wa muda mrefu kuhusu uchunguzi wa kweli".
No comments:
Post a Comment