VIONGOZI ARU WANOLEWA, WATAKIWA KUJIAMINI KATIKA NAFASI WALIZONAZO - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, April 17, 2024

VIONGOZI ARU WANOLEWA, WATAKIWA KUJIAMINI KATIKA NAFASI WALIZONAZO


Wakuu wa idara za kitaaluma, idara za kiuendeshaji na vitengo mbalimbali vya chuo Kikuu Ardhi (ARU) wamepatiwa mafunzo ya kiuongozi yenye lengo la kuwajengea uwezo na ufanisi ili kuboresha huduma na mazingira ya kujifunzia chuoni hapo.

Akizungumza wakati wa ufunguzi rasmi wa mafunzo hayo, Mwenyekiti wa Baraza la hicho Balozi Salome Sijaona,amewaasa viongozi hao kuwa na tabia ya kujiamini na kujiona wanatosha katika nafasi wanazotumikia pamoja na kutobabaika na kuondoa hofu katika kutimiza majukumu yao.

Balozi Sijaona ameongeza kwa, changamoto katika kazi ni jambo la kawaida, hivyo amewataka viongozi hao kutekeleza majukumu yote yenye manufaa na tija kwa taasisi wanayoiongoza Pamoja na kuwa na tabia ya kujitathimini wenyewe ili kutatua na kkuzuia changamoto katika maeneo ya kazi.

” Viongozi lazima watambue kuwa mafanikio yao yanatokana na watu wanaowaongoza,hivyo ni lazima wawe na tabia kufanya kazi kwa kushirikiana na watu wanaowaongoza ili kuleta matokeo Chanya katika taasisi”Aliongeza Balozi Sijaona.


Akimkaribisha mgenirasmi kufungua mafunzo hayo, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Ardhi, Prof Evarist Liwa amesema, sisi kama chuo tunaamini kuwa,ili kuleta mabadiliko katika taasisi ni lazima watu waongee na kusikiliza, hivyo tumeleta mafunzo haya ili viongozi muweze kutoa michango chanya na kupokea yale mtakayofundishwa na wawezeshaji wa mafunzo.
 
Mafunzo hayo yaliyoandaliwa na Chuo Kikuu Ardhi yanaendeshwa kwa kushirikiana na wawezeshaji toka kituo cha uwezeshaji viongozi(Uongozi Institute) yatafanyika tarehe 17 na 18 mwezi Aprili 2024, yatahusisha viongozi 61 wa idara za kitaaluma, idara za kiuendeshaji na vitengo vya chuo Kikuu Ardhi.

No comments:

Post a Comment