WAAJIRI WATAKIWA KUSAJILI MAENEO YAO YA KAZI OSHA. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Tuesday, April 23, 2024

WAAJIRI WATAKIWA KUSAJILI MAENEO YAO YA KAZI OSHA.

 

Na Okuly Julius , Dodoma .

 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu ( kazi ,Vijana ,ajira na watu wenye ulemavu) Deogratius Ndejembi amewataka waajiri wote nchini  kuhakikisha  wanasajili maeneo yao ya kazi OSHA pamoja na kuendelea kutekeleza taratibu mbali mbali za usalama na afya kwa mujibu wa Sheria Na. 5 ya Usalama na Afya Mahali pa kazi ya mwaka 2003.

 

Ndejembi ametoa kauli hiyo leo Aprili 22, 2024 jijini Dodoma , wakati akizungumza na waandishi wa habari kuelekea ,Siku ya Kimataifa ya Usalama na Afya  mahala pa kazi Duniani iyakayofanyika tarehe 28 Aprili 2024 jijini Arusha.

 

Aidha taarifa hiyo imeambatana na kauli mbiu isemayo Athari za Mabadiliko ya Tabia Nchi katika Usalama na Afya Kazini; Sajili eneo la kazi OSHA katika harakati za kupunguza athari hizo.

 

Lengo kubwa la maadhimisho haya ni kuendeleza kampeni za kuhamasisha na kuweka mazingirasalama katika sehemu za kazi miongoni mwa wadau kupitia kauli mbiu mbali mbali ambazo hutolewa na ILO.

 

Kauli Mbiu hiyo inalenga kuwakumbusha waajiri na wafanyakazi kwamba mabadiliko ya tabia nchi yanahusika kuzalisha vihatarishi vya usalama na afya mahali pa kazi kama vile kuongezeka kwa joto kali mahali pa kazi, majanga kama vile mafuriko kutokana na mvua zinazonyesha juu ya wastani nakadhalika,”

 

Mhe. Ndejembi ameongeza kuwa, “zaidi ya wafanyakazi milioni mia nne nambili (402,000,000) huumia wakiwa kazini nahivyo kushindwa kutekeleza majukumu yao kwa kipindi chote wanachopatiwa matibabu hadi hapo watakapopona. Kwa upande wetu hapa Tanzania jumla ya ajali na magonjwa yaliyoripotiwa katika Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi kuanzia Julai 2019 hadi Juni 2021 ni ajali 4,993 na magonjwa 249. Katika ajali hizo, vifo vilikuwa 217.

 

Sambamba na hilo ameelezea takwimu za kidunia zilizotolewa na Shirika la Kazi Duniani mwaka 2022 zinaonesha kwamba zaidi ya watu milioni mbili na laki tisa (2.9) hupoteza maisha kutokana na ajali na magonjwa yatokanayo na kazi na kuongeza takwimu hizo ni kubwa sana zinaathiri utendaji kwa kuwa zinasababisha upotevu wa maisha ya wafanyakazi na pia kuathiri shughuli wakati wafanyakazi walioumia wakiendelea kupata matibabu.

 

Amesema, serikali inatambua umuhimu wa kulinda nguvu kazi ya taifa na kupitia taasisi ya OSHA inaendelea kusimamia kwa karibu utekelezaji wa sheria Na. 5 ya Afya na Usalama Mahali pa Kazi ya mwaka 2003 miongoni mwa wadau na watanzania wote kwaujumla kuhakikisha kwamba maeneo yote ya kazi nchini yanakuwa na mifumo madhubuti ya kuwakinga wafanyakazi dhidi ya ajali na magonjwa yatokanayo na kazi.

 

Hata hivyo amebainisha kuwa serikali ikishirikiana na wadau wa Utatu inaendesha kampeni maalum ya uhamasishaji kupitia mafunzo na maonesho ya usalama na afya mahali pa kazi, bonanza la michezo miongoni mwa washiriki wa maonesho, kuandaa na kutoa tuzo za kuyatambua maeneoya kazi yanayotekeleza vyema sheria Na. 5 ya usalama na afya mahali pa kazi pamoja na kuhamasisha wafanyakazi kujumuika katika siku ya kilele kutafakari hali ya usalama na afya mahali pa kazi pamoja na kuwakumbuka wafanyakazi walioumia ama kupoteza maisha wakiwa wanatekeleza majukumu yao.

 

Maadhimisho ya siku ya usalama na afya mahali pa kazi yalianza kuadhimishwa mwaka 1998 nchini Marekani na madhumuni ya siku hii ilikuwa ni kuomboleza na kuwakumbuka wafanyakazi waliofariki kazini au kupata ulemavu wa kudumu kutokana na ajali pamoja na magonjwa huku maadhimisho hayo rasmi nchini Tanzania yalianza kuadhimishwa kwa mara ya kwanza mwaka 2004.



 

 




 

 

No comments:

Post a Comment