WAZIRI BASHUNGWA AWASILI DAR KUKAGUA ATHARI ZA MVUA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, April 29, 2024

WAZIRI BASHUNGWA AWASILI DAR KUKAGUA ATHARI ZA MVUA


Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa amewasili Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa, Albert Chalamila, kuanza ziara ya kikazi ya siku mbili mkoani humo leo Aprili 29, 2024.

Katika Ziara hiyo, Waziri Bashungwa atakagua miundombinu ya barabara, madaraja na maeneo mengine yaliyoathiriwa na mvua pamoja na kukagua hatua zinazoendelea kuchukuliwa na Mamlaka huska katika Sekta ya Ujenzi.

Waziri Bashungwa atatembelea barabara ya Kibada - Mwasonga, barabara ya Mji Mwema - Pembamnazi, barabara ya Kigamboni - Kibada, barabara ya Mwaikibaki, barabara ya Mbezi Vicktoria - Mpiji Magoe pamoja na utoaji huduma wa Vivuko vya Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA).

No comments:

Post a Comment