WAZIRI MKUU AKAGUA ATHARI ZA MAAFA RUFIJI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, April 17, 2024

WAZIRI MKUU AKAGUA ATHARI ZA MAAFA RUFIJI

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akizungumza na moja ya mwananchi aliopo katika kambi ya wahanga wa mafuriko iliyoka katika kata ya Chumbi Wilayani Rufiji Mkaoni Pwani.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mhe. Selemani Jafo ( kushoto) pamoja na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Ummy Nderiananga (kulia) wakati wa ziara ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa katika kata ya Chumbi Wilayani Rufiji Mkoani Pwani.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa(kulia) akipokea taarifa ya madhara ya mafuriko yaliyotokea Mkoani Pwani na hatua zilizochukuliwa na zinazoendelea kuchukulia kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani Bw. Abuubakar Kunenge (kushoto).
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim alipowasili kata ya Chumbi Wilayani Rufiji Mkoani Pwani kutoa pole na kuzungumza na Wananchi wa eneo hilo walipata madhara ya mafuriko ya Mvua zinazoendelea kunyesha Nchini.

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka wananchi waliokumbwa na adha ya mafuriko nchini waendelee kuwa watulivu wakati Serikali ikiendelea kuratibu utoaji wa misaada kwenye maeneo yaliyoathirika.

“Barabara ya Mkongo hadi Utete na ile ya kutoka Mloka Mkongo zote zimeathirika. Tunafanya kazi ya kurejesha mawasiliano ili wananchi waweze kupata huduma muhimu,” amesema.

Waziri Mkuu ametoa wito huo jioni (Jumanne, Aprili 16, 2024) wakati akizungumza na wananchi wa kata ya Chumbi, wilayani Rufiji, mkoani Pwani ambako alikwenda kukagua athari za mafuriko kwenye eneo hilo. Hadi sasa waathirika 740 wako kambini.

Waziri Mkuu ambaye aliwasili Ikwiriri, Rufiji akitokea Mlimba, Morogoro aliwaomba wananchi hao waendelee kutulia kwani serikali iko nao na itaendelea kuwahudumia hadi hali yao irejee katika hali ya kawaida.

“Naomba mpokee salamu za pole kutoka kwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, tunatambua kuna watu wamepoteza mali na wengine mifugo,” amesema.

Amewataka watendaji wa vijiji waendelee kubaini maeneo mapya ya kuishi ambayo yatatumika kuhamisha kaya zilizoathirika. “Watendaji wa vijiji tuainishe maeneo mapya ya kwenye miinuko ili baadaye watu waweze kuhamishiwa huko,” amesema.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu ameziagiza TARURA, TANROADS na TAZARA zishirikiane kufanya ukarabati katika maeneo yote yaliyopata athari wakati Serikali inasubiri kumalizika kwa mvua ili iweze kufanya ukarabati mkubwa.

Waziri Mkuu amefuatana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Dkt. Selemani Jaffo, Naibu Waziri wa Nchi (OWM-SBU) Bi. Ummy Nderiananga, Msemaji Mkuu wa Serikali, Bw. Mobhare Matinyi na watendaji wengine.

No comments:

Post a Comment