TANZANIA YATETA NA UONGOZI WA IDARA YA SERA ZA KIBAJETI - IMF-FAD - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, April 17, 2024

TANZANIA YATETA NA UONGOZI WA IDARA YA SERA ZA KIBAJETI - IMF-FAD

Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), akizungumza wakati ujumbe wa Tanzania ulipokutana na kufanya mazungumzo na Uongozi wa Idara ya Sera ya Kibajeti ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF-FAD), Kando ya Mikutano ya Majira ya Kipupwe (Spring Meetings) ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa IMF, inayoendelea Jijini Washington D.C nchini Marekani, ambapo pamoja na mambo mengine wamejadili namna ya kuimarisha ushirikiano kwa kutoa misaada ya kiufundi ili kuboresha mifumo na sera za kodi na ukusanyaji wa mapato ya Serikali.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, akizungumza wakati ujumbe wa Tanzania ulioongozwa na Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb) (hayupo pichani), ulipokutana na kufanya mazungumzo na Uongozi wa Idara ya Sera ya Kibajeti ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF-FAD), Kando ya Mikutano ya Majira ya Kipupwe (Spring Meetings) ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa IMF, inayoendelea Jijini Washington D.C nchini Marekani, ambapo pamoja na mambo mengine wamejadili namna ya kuimarisha ushirikiano kwa kutoa misaada ya kiufundi ili kuboresha mifumo na sera za kodi na ukusanyaji wa mapato ya Serikali.
Ujumbe wa Tanzania (kulia) ukiongozwa na Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb) (katikati) wakiwa katika mazungumzo na Uongozi wa Idara ya Sera ya Kibajeti ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF-FAD) (kushoto), Kando ya Mikutano ya Majira ya Kipupwe (Spring Meetings) ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa IMF, inayoendelea Jijini Washington D.C nchini Marekani, ambapo pamoja na mambo mengine wamejadili namna ya kuimarisha ushirikiano kwa kutoa misaada ya kiufundi ili kuboresha mifumo na sera za kodi na ukusanyaji wa mapato ya Serikali.
Naibu Mkurugenzi wa Idara ya Sera ya Kibajeti ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF-FAD), Bw. Abdelhak Senhadji, akizungumza jambo wakati ujumbe wa Tanzania ulioongozwa na Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb) (hayupo pichani), ulipokutana na kufanya mazungumzo na Uongozi wa Idara hiyo, Kando ya Mikutano ya Majira ya Kipupwe (Spring Meetings) ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa IMF, inayoendelea Jijini Washington D.C nchini Marekani ambapo pamoja na mambo mengine wamejadili namna ya kuimarisha ushirikiano kwa kutoa misaada ya kiufundi ili kuboresha mifumo na sera za kodi na ukusanyaji wa mapato ya Serikali.
Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), ( kushoto mstari wa mbele), akimsikiliza Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Bw. Lawrence Mafuru (kulia mstari wa mbele) wakati wa mazungumzo na Uongozi wa Idara ya Sera ya Kibajeti ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF-FAD) (kushoto), Kando ya Mikutano ya Majira ya Kipupwe (Spring Meetings) ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa IMF, inayoendelea Jijini Washington D.C nchini Marekani ambapo pamoja na mambo mengine wamejadili namna ya kuimarisha ushirikiano kwa kutoa misaada ya kiufundi ili kuboresha mifumo na sera za kodi na ukusanyaji wa mapato ya Serikali. Wengine katika picha ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba (katikati mstari wa mbele) na Viongozi waandamizi wa Wizara ya Fedha, Mamlaka ya Mapato Tanzania - TRA na Shirika la Fedha la Kimataifa-IMF walioketi mstari wa nyuma.

(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Washington DC)

Na . Joseph Mahumi, WF,Washington.


Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba (Mb), ameongoza Ujumbe wa Tanzania ulipokutana na kufanya mazungumzo na Uongozi wa Idara ya Sera ya Kibajeti ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF-FAD), Kando ya Mikutano ya Majira ya Kipupwe (Spring Meetings) ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa IMF, inayoendelea Jijini Washington D.C nchini Marekani ambapo pamoja na mambo mengine wamejadili namna ya kuimarisha ushirikiano kwa kutoa misaada ya kiufundi ili kuboresha mifumo na sera za kodi na ukusanyaji wa mapato ya Serikali.



Mkutano huo umehudhuriwa pia na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar, Dkt. Juma Malik Akil, Kamishna Msaidizi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania- TRA, Bw. Mcha Hassan Mcha, Viongozi waandamizi wa Wizara ya Fedha na Shirika la Fedha la Kimataifa-IMF.

No comments:

Post a Comment