YANGA SC WAFUNGIWA USAJILI WA NJE NA NDANI. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Tuesday, April 30, 2024

YANGA SC WAFUNGIWA USAJILI WA NJE NA NDANI.


Klabu ya Yanga SC imefungiwa na Shirikisho la Soka Duniani FIFA kufanya usajili wowote ule wa Mchezaji wa kimataifa kutokana na kushindwa kumlipa mshambuliaji wao wa zamani Lazaro Kambole.


Hayo yamekuja baada ya Mchezaji huyo kwenda FIFA kushtaki na kushinda kesi hiyo dhidi Ya Yanga SC.


Hivyo kutokana na FIFA kuifungia Yanga SC na TFF imeifungia kusajili Mchezaji yoyote yule kwenye Ligi ya ndani.





Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa umma na TFF imesema Kambole alishitaki Yanga kwa madai ya malimbikizo ya mshahara na fidia ya kuvunjiwa mkataba, ambapo timu hiyo ilipewa siku 45 kulipa pesa hizo na ilishindwa.


Taarifa hiyo imeeleza kuwa kushindwa kutekeleza hukumu ndani ya muda husika ndio sababu ya timu hiyo kufungiwa kusajili usajili wa ndani na wa nje.


Pia, Aprili 14, 2024, TFF ilitoa taarifa ya kufungiwa usajili klabu hiyo baada ya kukiuka Annexe ya 3 ya kanuni ya uhamisho wa wachezaji RSTP ya FIFA pamoja na kutokuingiza uthibitisho wa malipo ya uhamisho wa mchezaji (ambaye hakutajwa jina) katika usajili (TMS) licha ya kukumbushwa kufanya hivyo.


Hata hivyo, FIFA iliitaka Yanga kutekeleza matakwa ya kikanuni na kuwasilisha tarifa kwa sekretarieti ya Kamati ya Nidhamu ya FIFA ambapo suala hilo lilifikishwa kwa ajili ya hatua zaidi.


Yanga ilimtambulisha Kambole raia wa Zambia Juni 16, 2022 akitokea Kaizer Chiefs ambapo Septemba ,2022 iliachana na mchezaji huyo na kumpeleka kwa mkopo kwenye timu ya Wakiso Giant ya Uganda.


Kambole hakucheza mechi yeyote ya kimashindano akiwa ndani ya Yanga kwani alipata majeruhi katika mechi za kirafiki wakati timu hiyo ikijiandaa na msimu mpya wa 2022/2023.

No comments:

Post a Comment