Kampuni ya Apple inasema inafanya juhudi za haraka kurekebisha suala ambalo lilisababisha kengele[alarm} za iPhone kutotoa sauti, na kuwapa watumiaji wao waliolala kupitiliza kulilalamika.
Wengi, utumia simu zao kama kengele za alarm na baadhi ya walioathirika tu waligeukia mitandao ya kijamii ili kutoa kilio chao.
TikTokker mmoja alilalamika kwamba alikuwa ameweka " kengele{ alarm} tano" na hazikusikika.
Apple imethibitisha kuwa inafahamu suala hilo - lakini bado haijaeleza kile inachoamini kinasababisha, au nini watumiaji wanaweza kufanya ili kuepuka kuanza kuchelewa.
Haijulikani pia ni watu wangapi wameathiriwa au ikiwa tatizo limezuiwa kwa aina fulani za iPhone.
Wasiwasi huo hapo awali uliibuliwa na walioshiriki mapema kwenye kipindi cha Leo cha NBC, ambacho kilitoa taarifa hiyo.
No comments:
Post a Comment