AJUZA RAIA WA UKRAINE ATEMBEA KILOMITA 9 KUTOKA KIJIJINI KWAKE HADI ENEO SALAMA. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, May 2, 2024

AJUZA RAIA WA UKRAINE ATEMBEA KILOMITA 9 KUTOKA KIJIJINI KWAKE HADI ENEO SALAMA.

Lidiia Lomikovska alitenganishwa na familia yake walipokuwa wakijaribu kutoroka majeshi ya Urusi.


Lidiia Lomikovska mwenye umri wa miaka 98, uvamizi wa Urusi ni mbaya zaidi kuliko Vita vya Pili vya Dunia, ambavyo pia alikuwa alkiishi na amejifunza kuamini hisia zake.


Ndiyo maana majeshi ya Urusi yalipoingia kijijini kwao Ocheretyne mashariki mwa Ukraine, yeye na familia yake waliamua kuwa ni wakati wa kuondoka.


Hatahivyo, chini ya makombora mazito, Lidiia hivi karibuni alitenganishwa na jamaa zake, kwa hivyo akaanza kutembea magharibi "Nilichukua fimbo na ubao [kwa ajili ya msaada] na nikaenda zangu," aliiambia BBC. 


"Miguu yangu ilikuwa ikinibeba kwa namna fulani; sikuwa nimeibeba!"Alitembea kilomita 10 (maili 6) hadi alipochukuliwa na polisi wa Ukraine.


"Hakuna kitu kilichosalia! Kila kitu kiko juu chini!" alionekana akisema video iliyotolewa.


Kijiji alichoacha nyuma polepole kinabadilishwa kuwa mandhari ya kuzimu kila wanajeshi wa Urusi wanapokaribia .


Kadiri wanavyokaribia ndivyo mashambulizi ya vifaru yanavyozidi kuwa makali. Vyumba na nyumba zote zinageuka polepole kuwa vifusi na vumbi.

No comments:

Post a Comment