BIFU LA DAVIDO NA WIZKID KAMA DIAMOND NA KONDE. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, May 2, 2024

BIFU LA DAVIDO NA WIZKID KAMA DIAMOND NA KONDE.


Wanamuziki kutoka nchini Nigeria, Davido pamoja na Wizkid wapo katika bifu zito, baada ya shabiki wa Wizkid katika mtandao wa X (zamani Twitter) kumuomba msanii huyo atoe ngoma mpya ambapo Wizkid alimjibu kwa video ya Davido aliyokuwa akimlilia mwanadada Pink Native.


Kufuatia na video hiyo aliyoi-post Wizkid ndipo Davido akashindwa kuvumilia na kuanza kumrushia maneno kupitia mandao wa X kwa kumnanga Wizkid kuwa hana ngoma mpya inayotrend huku akidai kuwa ndiyo maana aliacha kuwekeza

mamilioni ya fedha kwa mtu ambaye amekufa kimuziki.


Hata hivyo Wizkid naye hakulikalia kimya ambapo aliamua kumjibu mkali huyo wa ngoma ya 'Unavailable' kuwa kwasasa hawezi kubishana naye ambapo alidai kuwa msanii huyo hawezi kufikia level zake hata akistaafu kufanya muziki leo.


Ikumbukwe kuwa wiki kadhaa zilizopita mwanadada kutoka nchini Marekani aliyejulikana kwa jina la Pink Native aliachia video kupitia mitandao yake ya kijamii ikimuonesha Davido akimlilia Pink ili waweze kuwa kwenye mahusiano.

No comments:

Post a Comment