Mchezaji na Kiungo wa Coastal Union Greyson Gwalala amemwaga wino na kuongeza mkataba wa miaka miwili wa kuendelea kuitumikia Coastal Union.
Mkataba wake una kipengele cha kuuzwa dirisha kubwa linalokuja kama atahitajika na timu yoyote kubwa ndani au nje ya nchi.
Timu itakayotaka huduma kutoka kwa Gwalala itabidi iongee kwanza na miamba hiyo ya Coastal Union yenye maskani yake jijini Tanga kabla ya kuongea na mchezaji kuhusu maslahi yake binafsi.
No comments:
Post a Comment