Jenerali Michael Langley Kamanda, Kamandi ya Marekani Afrika, akitoa ushahidi wakati wa kikao cha kamati ya Seneti kuhusu Huduma za kijeshi. |
Jeshi la Marekani linapanga kurejea Chad ndani ya mwezi mmoja kwa ajili ya mazungumzo kuhusu kurekebisha makubaliano ambayo yanairuhusu kubakisha wanajeshi huko, amesema jenerali mmoja wa Marekani.
Marekani ilisema mwezi uliopita ilikuwa ikiondoa askari wake wengi wa takriban wanajeshi 100 kutoka Chad baada ya serikali kutilia shaka uhalali wa operesheni zao huko.
Hii ilifuatia uamuzi wa Niger kuamuru wanajeshi wote wa Marekani kuondoka nchini humo, na kutoa pigo kwa operesheni za kijeshi za Marekani katika eneo la Sahel, eneo kubwa kusini mwa jangwa la Sahara ambako makundi yenye uhusiano na Al-Qaida na kundi la Islamic State yanaendesha shughuli zake.
Jenerali wa jeshi la Marekani la Marine Corps Michael Langley, kamanda wa Kamandi ya Marekani ya Afrika, alitoa maoni hayo kwa waandishi wa habari nchini Ghana katika Mkutano wa pili wa kila mwaka wa Vikosi vya Wanamaji barani Afrika, au AMFS.
Alisema uondoaji wa wanajeshi wa Marekani kutoka Chad unatarajiwa kuwa wa muda, na Chad imewasiliana na Washington kwamba inataka kuendeleza ushirikiano wa usalama baada ya uchaguzi wa rais nchini humo.
No comments:
Post a Comment