JIMBO LA MEXICO AMBAKO WAGOMBEA WANAPIGWA RISASI 'WANAPOTAFUTA KURA' - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, May 27, 2024

JIMBO LA MEXICO AMBAKO WAGOMBEA WANAPIGWA RISASI 'WANAPOTAFUTA KURA'

Cinthia Juarez anawania wadhifa huo mjini Acapulco baada ya rafiki yake, mwanaharakati maarufu wa haki za wapenzi wa jinsi moja, kuuawa kwenye kampeni.

Katika kile ambacho ni kampeni ya uchaguzi yenye vurugu zaidi katika historia ya Mexico, jimbo la magharibi la Guerrero ndilo eneo hatari zaidi nchini humo kutafuta kura.

Wachache wanaolitambua hilo bora kuliko Cinthia Juarez.

Mmoja wa watu wa kwanza kuuawa kwenye kampeni alikuwa rafiki yake wa utotoni, Moises "Moy" Juarez Abarca. Mwanaharakati maarufu wa kitaifa wa haki za wapenzi wa jinsi moja, Bw Abarca alikuwa mgombea wa serikali ya mtaa kupitia chama cha upinzani cha PRD kabla ya kutekwa nyara na watu wenye silaha.

Baadaye mwili wake ulipatikana umetupwa kwenye kaburi la pamoja na watu wengine 16.


“Nikiwa pamoja na rafiki yangu Moy, nimetumia zaidi ya miaka ishirini katika harakati za kisiasa. Hii imekuwa kampeni ya vurugu zaidi ambayo tumewahi kuona katika jimbo la Guerrero na Acapulco,” anasema Cinthia, ambaye amechukua nafasi yake kwa tiketi ya chama.


Huku mwenzake akiuawa na uchunguzi wa kesi yake kusitishwa, Cinthia anafahamu vyema hatari inayomkabiri kwa kugombea wadhifa wake. Lakini mwanamke huyo mdogo, mwenye dhamira kali, ambaye pia ni mtetezi mkuu wa haki za wapenzi wa jinsi moja katika jamii yake, anasema anakataa kuogopa.


“Bila shaka, ninaogopa. Ninaogopa kwamba siku moja nitaondoka nyumbani kwangu na sitarudi nyumbani, na itakuwa ni kutokana na sababu za kisiasa. Lakini siasa ndiyo njia pekee tunayopaswa kutumia kupaza sauti zetu, njia pekee ya kugeuza Acapulco kuwa bandari yenye kustawi ilivyokuwa hapo awali.”


Wakati uchaguzi unakaribia, ghasia zimezidi kuwa mbaya. Takriban watu 12 walipatikana wameuawa mjini Acapulco siku ya Jumanne, ikiwa ni pamoja na miili sita iliyogunduliwa kutupwa karibu na soko, siku chache kabla ya uchaguzi wa tarehe 2 Juni.


Na uchunguzi wa hivi majuzi wa kampuni ya ushauri ya kisiasa ya Meksiko, Integralia, unatoa picha mbaya ya ghasia za kisiasa kote nchini. Takriban watumishi 200 wa umma, wanasiasa na wagombea wameuawa au kutishiwa kipindi cha kuelekea uchaguzi wa Juni na kuna zaidi ya waathiriwa 50 huko Guerrero pekee.


Vurugu hizo zimeenea katika wigo mzima wa kisiasa, ingawa wagombea kutoka chama tawala cha Morena kitakwimu wameathirika zaidi.


Labda mauaji ya hali ya juu zaidi katika jimbo hilo yalifanyika Acapulco kabla ya Krismasi. Mmoja wa watu waliotarajiwa kuwa meya wa jiji, Ricardo Taja, aliuawa kwa kupigwa risasi alipokuwa akila chakula cha jioni katika mkahawa mmoja na mlinzi wake.


Vurugu za kisiasa zinazofanywa na wauzaji wa madawa ya kulevya si jambo geni nchini Mexico.


Lakini ukubwa wa tatizo katika kampeni hii umewashtua hata wanasiasa wa zamani hapa. Bw Taja alitarajiwa kufanya vyema katika uchaguzi huo iwapo angejihakikishia kuwania.


Majina yanaondolewa kwenye kura kupitia risasi - ikimaanisha kuwa baadhi ya wapiga kura watalazimika kuchagua wagombeaji wanaotumikia vyema zaidi maslahi ya uhalifu uliopangwa badala ya mahitaji ya jamii zao.


Cinthia Juarez aliipeleka BBC kuvinjari baadhi ya biashara za ndani na Evodio Velazquez. Meya wa zamani wa Acapulco, Bw Velazquez anasema amevumilia vitisho dhidi yake maisha yake yote ya kisiasa.


Alipokuwa akigombea ubunge katika uchaguzi huu, watu wenye silaha walitokea nyumbani kwake na kutaka kumuona, kwa kitendo cha kumtisha.


Tangu wakati huo ameacha mbio za kisiasa.


"Ni afadhali kuwa salama kuliko kuuawa", anasema. "Sitaki kuwa takwimu nyingine ya mauaji."


Meya wa zamani anasema alikuwa amewasiliana na mamlaka ya shirikisho ili apewe maelezo ya usalama lakini ombi lake "lilianguka kwenye masikio ya viziwi. Hawajachukua hatua hata kidogo."


Evodio Velazquez alijiondoa kwenye uchaguzi baada ya watu wenye silaha kujitokeza nyumbani kwake.


Bw Velazquez anasema kampeni hii ya umwagaji damu nyingi zaidi ya uchaguzi imesababisha "kutokuwa na uhakika na hofu katika jamii" akilaumu "sera zilizofeli za umma katika suala zima la usalama".

Kwa hakika, wapiga kura katika jimbo hilo wana uwezekano wa kumchagua tena mmoja wa watu wenye utata katika siasa za Meksiko, Seneta Felix Salgado Macedonia.

Seneta huyo alilazimika kujiondoa katika kinyang'anyiro cha ugavana mwaka wa 2021 kwa madai ya ubakaji na unyanyasaji wa kingono. 


Alikanusha mashtaka na kesi dhidi yake hatimaye ikatupiliwa mbali.


Katika kashfa hiyo yote, alitegemea uungwaji mkono usioyumba wa Rais Andres Manuel Lopez Obrador.


Kura rasmi zinaonyesha karibu asilimia sitini ya watu wa Mexico wanachukulia miji yao si salama. 


Seneta Salgado Macedonia anasisitiza kuwa hayo ni maboresho katika miaka iliyopita. Pia anakanusha mkakati wa Rais wa usalama - ambao mara nyingi hufupishwa na nukuu yake "abrazos, no balazos", ikimaanisha "kukumbatia, sio risasi" - imeshindwa:


"Nukuu hiyo lazima iwekwe katika muktadha", anasema. "Rais alikuwa akisema kwamba huko Mexico tunataka kuona kukumbatiwa, sio risasi. 


Kwamba tunatakiwa kushughulikia vyanzo vya ukatili ikiwemo umaskini na kuvunjika kwa familia.”




Seneta Felix Salgado Macedonia anatarajiwa kushinda kinyang'anyiro hicho, baada ya kujiondoa 2021 kufuatia mashtaka ambayo sasa yametupiliwa mbali ya unyanyasaji wa kingono.


Hata hivyo, alikiri kwamba huko Guerrero na kote nchini kuna kazi kubwa mbele ya yeyote atakayeshinda tarehe 2 Juni. 

Mgombea wa chama chake, Claudia Sheinbaum, ndiye yuko katika mchujo wa kuwa rais wa kwanza mwanamke wa Mexico.

"Tunapaswa kusonga mbele kidogo kidogo hadi tufanikishe utulivu wa nchi nzima," anasema Seneta Salgado. "Lakini tuna shida nyingine: jirani yetu mkubwa wa kaskazini. Ili dawa zinunuliwe na kuuzwa, lazima kwanza kuwe na usambazaji na mahitaji. 


Kwa hiyo, nani anatumia dawa hizo?”

Watu huko Acapulco wamevumilia mwaka mgumu sana.


Miezi minane iliyopita, Kimbunga Otis kiliingia katika jiji la pwani kwa nguvu kubwa. Uharibifu uliosababishwa na dhoruba ya aina ya tano bado unaonekana kutoka kwa vyumba vilivyoharibiwa vilivyo karibu na ufuo hadi vitongoji vya mapato ya chini.


Mercedez Sanchez alipoteza zaidi ya wengi. Analia huku akieleza jinsi mama yake na kaka yake wote walivyozikwa chini ya maporomoko ya ardhi, mitaa michache tu kutoka kwenye nyumba yake ya kawaida katika kitongoji cha Francisco Villa.



Mercedes alipoteza mama yake na kakake baada ya Kimbunga Otis kupiga Acapulco.


Mercedes anasema kutoa chakula, msaada wa moja kwa moja wa kifedha wa karibu $3,000 (TSh7,791,489.22) kwa kila kaya na hata vifaa vingine vya nyumbani ni changamoto kubwa.

Lakini wakati Acapulco inaanza kujikwamua tena baada ya dhoruba, hali yake ya usalama bado ni mbaya: hakuna siku inayopita katika jiji bila mauaji.


Maeneo machache tu, mwathiriwa wa hivi punde zaidi alikuwa dereva wa teksi, aliyepigwa risasi akiwa anasubiri wateja, mkanda wa polisi wa manjano ukiwa bado umezingira eneo la uhalifu na madoa ya damu yakionekana barabarani.


Siku ya kupiga kura inapokaribia, Mercedez anasema uhalifu wa mara kwa mara utaathiri uamuzi wake wa mwisho. Maisha ya kila siku katika jamii yake yamejaa hatari.


“Hatuwezi hata kutoka nje bila woga. Hata kama hutafuti shida, unaweza kuwa mahali pasipofaa kwa wakati usiofaa. Ni hatari kila wakati.”

No comments:

Post a Comment