KUTOKA MAHAKAMA YA WILAYA YA KALIUA MKOANI TABORA. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, May 25, 2024

KUTOKA MAHAKAMA YA WILAYA YA KALIUA MKOANI TABORA.



Mei 24, 2024 katika Mahakama ya Wilaya ya Kaliua mkoani Tabora mbele ya Mh.  Felix Ginene Hakimu Mkazi Mwandamizi, imeamriwa kesi ya Jinai Na.71/2023 Jamhuri dhidi ya  Richard Maganga Mpagama na Laurent Isaya Sendu.


Watu hawa wametiwa hatiani kwa kosa la kuomba na kupokea hongo ya Tsh. 3,000,000/=  k/f 15(1)(a)na (2) cha PCCA (Sura ya 329 marejeo ya Mwaka 2022)


Kwamba mnamo tarehe 21/04/2023 watuhumiwa Richard Maganga Mpagama akiwa ni Mtendaji wa Kijiji cha Imagi, Kata ya Nh'wande na Laurent Isaya Sendu, Mtendaji wa Kata ya Nh'wande Wilayani  Kaliua Mkoani Tabora, waliomba  rushwa Tzs 3,000,000 kutoka kwa mwananchi mkazi wa kijiji cha Imagi, Kata ya Nh'wande Wilayani Kaliua Bw. Ndilana Budeba Ili wamwachie huru na aishi kwa amani katika kijiji hicho kwa kosa alilounganishwa lililomhusu mkwe wake (mume wa binti yake) kuhusika na wizi wa kutumia silaha.


Kesi iliongozwa na waendesha Mashtaka wa Serikali David Bakari pamoja na Kajivo Aidan.


Washtakiwa wametiwa hatiani na kuhukumiwa kwenda jela miaka mitatu au kulipa faini ya sh. 1,000,000/= kila mmoja na kuamriwa kumrejeshea Ndilana Budeba kiasi cha sh. 2,300,000/= ikiwa ni sehemu ya fedha iliyobaki baada kumrejeshea kiasi cha sh. 700,000/= wakati uchunguzi ukiwa unaendelea.


Washtakiwa wameshindwa kulipa faini na hivyo wamepelekwa gerezani.

No comments:

Post a Comment