Na WyEST , London Uingereza
Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda amewasilisha Mada juu ya mageuzi ya Elimu Tanzania na kuwakosh wajumbe wa Mkutano wa Elimu Duniani unaofanyika London Uingereza.
Tanzania inashiriki katika Mkutano huo ulioleta pamoja nchi zaidi ya 200 Duniani kujadili maendeleo ya Elimu Duniani ikiwa ni nguzo kuu ya kuandaa Rasilimali watu wenye ujuzi ma mtaji mkubwa katika kuleta maendeleo.
Katika Wasilisho Prof. Mkenda ameelezea namna Tanzania ilivyoanza kazi ya utekelezaji mageuzi kwa kufanya mitaala kulenga elimu ujuzi na kusisitiza umuhimu wa wadau wa elimu wakajielekeza katika kutatua changamoto kimfumo ikiwemo ugharamiaji, vifaa, walimu bora na ujuzi.
Baada ya wasilisho hilo Mkenda pia ameshiriki
katika Jukwaa la elimu kama mmoja wa wachangiaji kuhusu nini kifanyike kuwianisha Elimu jumla na amali ili kuandaa wahitimu wataokidhi mazingira ya ajira na maisha ya kazi kwa ujumla.
No comments:
Post a Comment