Mahakama kuu ya Umoja wa Mataifa ICJ imeamuru Israel kusitisha operesheni yake huko Rafah mara moja.
Mahakama hiyo aidha imeitaka Israel kufika mbele yake ndani ya mwezi mmoja kuelezea jinsi inavyotekeleza maagizo yake ikiwa ni pamoja na Israel kufungua kivuko cha Rafah na Misri ili kuruhusu misaada ya kibinadamu.
Hii ni mara ya kwanza kwa ICJ kutoa uamuzi unaoilazimu Israel kubadili kwa kiasi kikubwa operesheni yake ya kijeshi huko Gaza.
Jopo la majaji wa kimataifa lilisema kuwa Israel haikuwashawishi kwamba juhudi za kuwahamisha wakazi wa Rafah na operesheni zake zinalenga kuimarisha usalama wa raia katika Ukanda wa Gaza.
Afrika Kusini ilikuwa imewasilisha kesi katika mahakama hiyo kutaka Israel iamrishwe kusitisha kwa dharura kwa mashambulizi yake huko Rafah.
Afrika Kusini ilisema haki ya ulinzi ya Wapalestina chini ya mkataba wa mauaji ya halaiki, ulioanzishwa 1948 ilikuwa katika hatari ya kukiukwa na kuitaka ICJ uingilia kati.
No comments:
Post a Comment