MALORI ELFU MBILI YA MISAADA YAKWAMA KWENYE MPAKA WA RAFAH - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Friday, May 24, 2024

MALORI ELFU MBILI YA MISAADA YAKWAMA KWENYE MPAKA WA RAFAH



CHANZO NI BBC SWAHILI


Msaada wa kibinadamu huko Gaza "umelemazwa kimfumo" na vikwazo vilivyowekwa na pande zinazopigana huko, linaonya shirika la Wakimbizi la Norway.


Shirika hilo limesema malori 2,000 ya misaada yamekwama kwenye upande wa Misri wa kivuko cha mpaka cha Rafah, ambacho kimefungwa tangu jeshi la Israel lianzishe operesheni dhidi ya Hamas katika mji wa kusini wa Rafah tarehe 6 Mei.


Suze van Meegen, mkuu wa operesheni wa NRC huko Gaza, alisema Wapalestina "wananyimwa" shehena zinazohitajika sana za dawa, mahema, matangi ya maji, bidhaa za usafi na mambo mengine ya msingi.


Jeshi la Ulinzi la Israel (IDF) linasema kuwa limefungua vivuko vipya, barabara za lami na kuweka mabomba ya maji ili kupunguza mateso ya Wapalestina, na linadai kuwa watu milioni moja waliokimbia makazi yao wamehama kutoka Rafah, kabla ya mapigano

No comments:

Post a Comment