CHANZO NI IDHAA YA KISWAHI - DW
Ziara ya Ruto ndiyo ya kwanza ya kiserikali kufanywa na rais wa Afrika katika Ikulu ya White House tangu 2008, na inaashiria umuhimu wa bara hilo ambalo watu bilioni 1 lina uhusiano wa karibu wa kibiashara na China, lakini likiwa nyuma ya vita vya Ukraine na Gaza kwenye ajenda ya Washington.
Siku ya Alhamisi jioni, Ruto alikuwa mgeni rasmi katika dhifa ya chakula cha jioni iliyovutia wageni mbalimbali, kuanzia mwimbaji na mtunzi wa nyimbo Don McLean hadi kamishna wa NFL Roger Goodell, Wakurugenzi Wakuu wa Walmart na Pfizer pamoja na Rais wa zamani Bill Clinton. Rais wa zamani Barack Obama, ambaye babake alikuwa Mkenya, alijitokeza kwa muda mfupi kabla ya chakula.
"Tunaweza kutenganishwa na umbali, lakini tumeunganishwa na maadili sawa ya kidemokrasia," Biden alisema wakati akimsalimia Ruto kwenye bustani ya Ikulu. Biden alikumbusha kuhusu ziara zake mwenyewe nchini Kenya akiwa kijana, akipongeza uhusiano wa kidiplomasia wa miaka 60 kati ya nchi hizo mbili baada ya uhuru wa Kenya.
"Ziara yangu inafanyika wakati ambapo demokrasia inachukuliwa kuwa inarudi nyuma duniani kote," Ruto alisema, akiwa amesimama na Biden, Makamu wa Rais Kamala Harris na maafisa wengine wa baraza la mawaziri. Hapo awali, alikuwa amekutana kwa faragha na Biden katika Ofisi ya Oval.
"Tulikubaliana kuhusu fursa muhimu kwa Marekani kurekebisha kwa kiasi kikubwa mkakati wake na kuimarisha uungaji mkono wake kwa Afrika," Ruto alisema.
Biden alisema ataiteua Kenya kuwa nchi ya kwanza ya Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara kuwa mshirika mkuu asiye wa NATO. Qatar, Israel na nchi nyingine 16 zinashiriki hadhi hiyo. Nairobi na Washington zinashikirikiana katika mapambano dhidi ya ugaidi barani Afrika, utulivu nchini Haiti na kuiunga mkono Ukraine.
No comments:
Post a Comment