MIFUMO KANDAMIZI INAYOENDELEA KATIKA JAMII INACHOCHEWA NA MILA NA DESTURI - DKT. GWAJIMA. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, May 15, 2024

MIFUMO KANDAMIZI INAYOENDELEA KATIKA JAMII INACHOCHEWA NA MILA NA DESTURI - DKT. GWAJIMA.

 


Na Carlos Claudio, Dodoma. 

 

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima amesema mifumo kandamizi inayoendelea katika jamii inachochewa na mila na desturi zenye madhara kwa baadhi ya makabila  zimesababisha wanandoa hasa wanawake kukaa kimya bila kujadili na kumaliza tofauti zao jambo ambalo limechangia ndoa nyingi kuvunjika au wenza kutengana. 

 

 Waziri Dkt. Gwajima ameyasema hayo leo Mei 15,2024 Jijini kwenye Maadhimisho ya Siku ya Familia Duniani yaliyoambatana na uzinduzi wa mpango kazi wa taifa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto awamu ya pili (MTAKUWWA II) na kuongeza kuwa kiwango hicho kinapungua lakini bado ni kikubwa kwa wanawake na watoto.

 

"Kati ya vikwazo katika kukabiliana na migogoro ya familia ni kukosekana kwa upendo, ustahimilivu na kutokuwa na hofu ya Mungu miongoni mwa wanafamilia, tabia zote hizi ni matokeo mojawapo ya ukosefu wa malezi na makuzi mema katika umri wa awali",amesema. 

 

Aidha, ameongeza kuwa kwasasa kwa upande wa wanawake walioolewa, vitendo vya unyanyasaji wa kimwili, kingono, au kihisia vimepungua kutoka 50% mwaka 2015/16 hadi 39% mwaka 2022/23.

 

Amesema, Vikwazo vingine ni mawasiliano duni miongoni mwa wazazi au walezi na watoto ambapo athari zake ni watoto kukosa upendo kwa wazazi au walezi unao sababisha kukosekana kwa muunganiko yaani bond kati ya wazazi au walezi na watoto.

 

Dkt. Gwajima ameongeza kuwa katika kipindi cha Julai 2023 hadi Aprili 2024, Wizara na Wadau kupitia Mwongozo wa Taifa wa Wajibu wa Wazazi na Walezi Katika Malezi ya Watoto na Familia imeendelea kutoa elimu ya malezi chanya kwa jamii kupitia redio na runinga, mikutano na makongamano yanayohusisha wananchi na mitandao ya kijamii. 

 

Naye Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mohamed Mchengerwa amewaagiza wakuu wa mikoa kuzungumzia masuala ya adhabu zinazotolewa pindi mtu anapofanya vitendo vya ukatili pale wanapokutana kwenye vikao vyao.

 

"Adhabu zinazotolewa zinapaswa kuendana na kosa ambalo mtu amefanya kuliko kupewa adhabu ambazo kosa lililofanyika ni mkubwa lakini adhabu haziendani na kosa na pengine ukuta mtu yupo tu mtaani anaendelea na kazi zake huku muathirika akiendelea kuteseka",amesema. 

 

Waziri wa Katiba na Sheria Balozi Dkt.  Pindi Chana amesema Wizara ya katiba na sheria ni mdau mkubwa wa kutoa haki kwa watu wote hasa kwa wanawake na watoto wanaopitia ukatili na kukosa msaada wa kisheria.

 

"Tutahakikisha kila mtu mwenye changamoto ya kisheria anapata msaada nchi nzima na kuna namba maalum ya kuwasiliana nasi na wapo manasheria wetu ambao kazi yao ni kutoa msaada na watu wasijichukulie sheria mkononi waende kutafuta huduma kwasababu zinatolewa bure. 

 

Awali akizungumza katika maadhimisho hayo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Theopista Mallya ameiomba serikaki wanaobaka watoto chini ya miaka Kumi wasidhaminiwe kutokana na kuwepo kwa ongezeko kubwa la watoto wadogo kubwakwa.




No comments:

Post a Comment