Ashrack Miraji Same Kilimanjaro
Katibu Tawala wilaya ya Same Upendo Wella ameyasema hayo wakati akimwahakilisha mkuu wa wilaya ya Same Kaslida Mgeni kwenye kuhitimisha umoja wa michezo na taaluma shule za sekondari Tanzania (UMISETA).
“Nidhamu ni jambo la msingi sana katika michezo, hivyo niwaombe wanafunzi ambao mnakwenda kushiriki mashindano hayo kwenye ngazi ya mkoa kuwa na nidhamu, hasa kwa kile unachofundishwa na kuheshimu kila mtu ambaye utakutana naye kwenye michezo.”
Sambamba na hilo, “niwaombe pia wanafunzi ambao mnashiriki Mashindano ya UMISETA, kuendelea kujikita zaidi kwenye masomo yenu ili kutimiza ndoto zenu kwenye maslahi mapana ya Taifa letu,” amesema Wella.
Amesema kuwa michezo inaambatana na elimu, kwani baadhi ya vijana ambao wanashiriki kwenye michezo mbalimbali wamepata mafanikio makubwa.
Aidha amewasisitiza walimu, wafanyakazi, na wanafunzi kudumisha na kuendeleza michezo kwa maana michezo ni afya, ajira na hudumisha mahusiano mazuri kwa vijana wetu.
Na kuongeza kuwa michezo inaleta maendeleo makubwa katika Taifa pia Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, anatoa hamasa kwa timu za hapa nchini kwenye mashindano tofauti ndani na nje ya nchi.
No comments:
Post a Comment